Wema Sepetu ataka kugombea ubunge

Tanzania zaidi ya uijuavyo......ukishangaa ya Musa utastaajabu ya firauni
 

Ndugu, mi hapa nitatofautiana na ww. Hivi kwakuwa tayari tuna wabunge kadhaa 'vilaza' ni sahihi kuendelea ku-entertain 'vilaza' wengine? Ni kweli kila mtu ana udhaifu wake, kitu cha msingi ni je anataka kuwafanyia nini watz? Atafanya nini ile aweze kutekeleza? Amefanya nini so far ili kuweza kuwaondelea kero wananchi? Sio lazima uwe mbunge ili uweze kutetea kero mbalimbali za wananchi. Je yeye amewahi kutoa tamko au kufanya kitu cha kuwatetea wananchi? Nitakupa mfano wa Mnyika ambaye licha ya 'kushindwa' 2005, bado alikuwa bega kwa bega na wananchi wa jimbo lake-mfano kushughulikia matatizo ya ardhi.

Kuna wakati nilimsikia Mzee Yusuph akiahidi kugombea ubunge huko mbeleni. Akadai kama anaweza kutunga nyimbo za kuwagusa watu wengi kwa kiasi kikubwa, hawezi shindwa kujua matatizo yao na kuyatatua. Wasiwasi wangu ni watu kutumia umaarufu usiohusiana na uongozi moja kwa moja kutaka kuwawakilisha wananchi. Hatujui watu hawa wana msimamo gani kuhusiana na mambo ya kitaifa kama katiba mpya, unyanyasaji unaofanywa na polisi kwa raia, umaskini, n.k. Lazima mtu achaguliwe kwa uwezo wake wa kuongoza, maono,uadilifu na uzalendo. Kwa jinsi upepo unavyovuma, wabunge wanaosafiria nyota za fani zingine,watayeyuka kama siagi juani.
 
Wema ni easy taker sana. Hawezi kujadili mambo ya msingi katika Bunge la sasa. Tunataka watu wanaoweza kufanya maamzi yenye tija sio kuendekeza starehe na matanuzi...
 
Duh,koment zako tu kimwana mimi hoi.............yaani nshaku feel kama vile tumeshaonana siunajua....Acta exteriora indicant interiora secreta??????
Hhahah...Mvua ya kiangazi aka manyunyu!!Hizo lugha zenu sielewi au ni ujumbe wa Wema?!
 
Baba yake anamu-inspire, je yeye kama yeye wito wake ni nini? Amepanga kuwasaidia nini waTZ au ana nia sura yake ionekane tu mjengoni kwa sababu alishazoea umaarufu? Kama ana nia ya dhati basi ajivue kwanza gamba la tabia zake mbaya atafanikiwa. Kila la kheri
 
Wema ni easy taker sana. Hawezi kujadili mambo ya msingi katika Bunge la sasa. Tunataka watu wanaoweza kufanya maamzi yenye tija sio kuendekeza starehe na matanuzi...

Hao walioko bungeni, hasa hasa wale wa chama cha magamba amabo wengi wao ni wazee na wastaafu, wanafanya nini cha maana? Kazi yao kugonga meza na kusinzia tu! Bora hata Wema ana damu changa anaweza kuleta changamoto.

Amina Chifupa (RIP) alipotangaza nia yake ya kugombea Ubunge watu walimbeza sana. Lakini alishinda, na alipofika bungeni alitoa changamoto. Hali kadhalika Mr II pia watu walimbeza sana. Sasa hivi yuko mjengoni!
 
Nauliza hivi kuna mpango wa kuanzisha Wabunge wa vitanda maalum mwaka 2015 ?
 
Hhahah...Mvua ya kiangazi aka manyunyu!!Hizo lugha zenu sielewi au ni ujumbe wa Wema?!
teh teh teh..........acta exteriora idicant interiora secreta=external actions show internal secrets,ndio nilimaanisha hivyo tu,pole kwa usumbufu....................
 
teh teh teh..........acta exteriora idicant interiora secreta=external actions show internal secrets,ndio nilimaanisha hivyo tu,pole kwa usumbufu....................
Uhakika ni bora kuliko hisia...sasa nimekusoma!!Enhe hiyo secreta ndo ipi embu nijulishe...,
 
Kama akina Maji Marefu na akina Livingstone walipata Ubunge, ni dhahiri kuwa akigombea kupitia CCM katika jimbo lolote la vijijini mikoa. Fulani ya pwani na michache ya kati atapata tu
 
huyu akijipitisha tu kwa anayechekacheka ubunge anao wala hata asipogombea
 
ahaaa wala asigombee atapata kiti kile
cha viburudisho teheteheteheeee
 
Labda ubunge wa umalaya ndiyo utapata ukawawakilishe bunge lao lakinia siyo hili la watu makini.

acheni kumrudisha nyuma kwa kumpiiiiiiiinga hivyo,mbona tofauti yake na wengine waliopo kule ndani ni ndogo tu?
 
Only in bongo kila mzushi anaeza kuwa mwanasiasa.
Si kweli Jay Z naye amesema anampango wa kugombea urais marekani katika miaka sita ijayo, jayz ni mchafu kuliko wema, ameuza madawa ya kulevya nyimbo zake zinatetea vitendo vya kimalaya na haamini mungu.
 

Mh labda chama cha magamba...maana huko ndio wanaangalia sura kuliko uwezo wa mtu,hasa kwa wanawake.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…