Wema Sepetu: Kupendeza Muhimu lakini Kuelimika ni muhimu zaidi

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Bi dada Wema Sepetu ambae ni mwigizaji katika tasnia ya Bongo Movie amefunguka na kuweka wazi kuwa urembo au kupendeza tu haitoshi katika maisha ya binadamu bali jambo kubwa na la msingi katika maisha ni kupendeza na pia kuongeza maarifa katika

Wema Sepetu akipata maarifa.
nyanja mbalimbali ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupambana na vikwazo pindi unapokutana nayo,Wema Sepetu amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Inst gram.

Wema Sepetu amewataka watanzania kujifunza na kuongeza maarifa mbalimbali kwani elimu haina mwisho hivyo si vibaya kama watajitolea muda wao kuongeza maarifa kwani yeye anakili wazi kuwa anajifunza vingi katika maisha ya kila siku,maana kupendeza tu haisaidii kama hutakuwa na elimu ya mambo mbalimbali.

"Kupendeza ni muhimu ila kuelimika ni muhimu zaidi.Je, unajaribu kujifunza kitu kipya kila siku? Elimu haina mwisho na Mimi binafsi najifunza mengi kwa kaka angu Mr problem solved.Jitahidi kujiendeleza kimawazo na hautakwama ukikutana na vikwazo"

Mbali na hilo pia Diva huyo wa bongo Movies ameonyesha kuwa ni #ZamuYako2015 kufanya jambo ambalo litabadili maisha yako na kuweka historia nyingine katika maisha yako kwa kuthubutu na kufanya mabadiliko chanya yenye lengo la kuinuana kama vijana.

"Huu ni mwaka 2015. Kama kupendana bure, tushapendana vya kutosha. Kama kutukanana bila sababu, tushatukanana vya kutosha. Kama kushabikia vitu ambavyo havina msaada wowote kwa sisi na familia zetu,tushashabikia vya kutosha.Imefika hatua ya kunyanyuana,sio kushushana.Kuelimishana,sio kusemana.Kupeana moyo,sio kukatishana tamaa."

"Imefika hatua ya kutegemea mabadiliko, na kupigania mabadiliko.Nakuomba wewe kaka angu, dada angu, mama angu, baba angu...nakuomba ufanye maamuzi leo, kwamba kesho yako haitakua kama jana yako.Kwa jina naitwa Wema Sepetu. Na leo hii nimeamua kwamba kesho yangu, haitakua kama jana yangu!"Aliongeza Wema Sepetu.

Chanzo:EATV
 
Wabongo tunapenda kukatishana tamaa sana. . . Hata kama angekuwa na miaka 50 bado si sawa kumkatisha tamaa. . . .Huo ni ujumbe muhimu sana kwa wenye akili! Ifikie hatua tuweke chuki binafsi pembeni na tusapoti maendeleo

Hiyo akili Hakuwa Nayo Mwanzoni.???.. Husia Huja baada Ya Maisha Kukaribia Kifooo...

Ukiwa Mpenda Starehe na Umezungukwa Na Walevi Hutakumbuka Kuandika Hayooo. Ila Baadae majuto mjukuu ndo anakuja
 
Wabongo tunapenda kukatishana tamaa sana. . . Hata kama angekuwa na miaka 50 bado si sawa kumkatisha tamaa. . . .Huo ni ujumbe muhimu sana kwa wenye akili! Ifikie hatua tuweke chuki binafsi pembeni na tusapoti maendeleo

Shangaa na wewe.
Mtu hata miaka 30 hafikishi eti amechelewa, kachelewa wapi sasa!!!

Alijiimbiaga Ally Kiba, kwa binadamu huonekani mwema mpaka wema wayaseme mema!

So far Wema kaongea mambo ya msingi sana kazi kwake tu kuyahamishia kwenye vitendo.
 
Hiyo akili Hakuwa Nayo Mwanzoni.???.. Husia Huja baada Ya Maisha Kukaribia Kifooo...

Ukiwa Mpenda Starehe na Umezungukwa Na Walevi Hutakumbuka Kuandika Hayooo. Ila Baadae majuto mjukuu ndo anakuja

Hivi mliambiwa Wema ni malaika?
Wewe mambo yako yote umeyafanya kwa wakati?
Haukuwahi kupotoka mahali na kufanya makosa katika maisha yako?

Come on dude, reduce that state of being too judgemental!!!"
 
Ameongea jambo la busara sana, ila katika kujifunza kwake ajifunze pia vipodozi vikali na unywaji wa pombe ulopitiliza husababisha kansa.
 
Hold on a little bit.....
Kwahiyo kama kachelewa ndo haruhusiwi kuyaona/kufanya mazuri?

Hakunaga kitu kama hicho!

Sasa Tatizo lipo wapi mi si Nimesema Kachelewa.... Wewe sema Kawahi Ili Ubalance Basi...

Mi nimeona Hivyo maaan huko Nyuma Angetakiwa Kufanya Hayo...... ila Kachelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…