WEMA SEPETU mtoto wa kiislam huyupo hivyo!

tenanzinyo

Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
64
Reaction score
23
Habari wana JF wenzangu hopeful mpo poa!
Jana usiku nlikuwa natazama kipindi cha THE MBONI SHOW katika kituo cha runinga namba 1kwa vijana Tanzania EATV chini utangazaji wa mwanadada MBONI MASIMBA ambapo katika kipindi huwa ana walika wegeni tofauti tofauti kuzungumza mada mbalimbali za kijamii,kiutamaduni,kimapenzi nk.

Kwa show ya jana alikuwa na bongo moves star Wema Isack Abraham Sepetu wakijadili mada ya Uwazi katika Mapenzi ambapo mwanadada Wema bila kupepesa macho wala kutafuna maneno alitiririka kinagaubauga kuhusu maisha yake ya kimahusiano ya mapenzi,ambapo aliwataja wanaume wote ambao kwa nyakati tofauti amedate nao.

Wanaume wao ni pamoja na Marehemu Stephen Kanumba,Jumbe,TID,Mr Blue,Chalz Baba na hivi karibuni Dimond Platinum"sukari ya warembo"Kwanza niseme nlikuwa sifahamu kama Wema ni Binti wa kiislam!ila ni katika show hiyo ya jana nlifahamu kutokana na Wema mwenyewe kujiita mtoto wa kiislam pale alipokuwa anajitetea au kujibu maswali aliyokuwa akibanwa na aidha wanaalikwa kwenye show au host wa kipindi Mboni Masimba.

Lengo la thread hii siyo kuutazama na kujaji uislamu wa Wema ila kilichonisikitisha ni jinsi Wema alikuwa anajificha katika kivuli cha mwamvuli wa dini ya kiislam kwa mambo mbalimbali aliyokuwa akiulizwa!Ni ukweli usiopingika kuwa matendo anayofanya Wema ni kinyume kabisa na mafundisho ya dini ya kiislamu au jinsi binti wa kiislamu anatakiwa aishi,mojawapo ikiwa ni hilo la kukiri kufanya zinaa na wanaume zaidi ya watano kabla ya ndoa tena hadharani.

Ni aibu kubwa Wema Kujivunia uislamu wake wakati matendo yake yapo kinyume kabisa na mafundisho ya dini hiyo!

Wito wangu kwa dada Wema na mastar wengine ambao wana majina ya kiislam waache haka katibia cha kujiita mtoto wa kiislam wakati dhahiri shahiri metendo,tabia na maadili yao haviendani na mafundisho ya dini ya kiislamu kwani wanaidhalilisha uislam na waislamu ni vyema wakakaa kimya tu wasifiche uchafu wao kwa kujiita watoto wakiislamu!Uislam kama dini ni mfumo mzima wa maisha wenye maadili sheria na taratibu zake ambazo Wema anatakiwa kuzifuata kabla ya kujinadi kuwa yeye ni mtoto wa kiislam!

Mwisho napenda kumsihi dada yangu Wema kumrejea Muumba Wake kama ilivyoamrishwa ktk kitabu chao kitakatifu cha Quran!
 
Nadhani lengo lako unataka tuingie katika mtego wa kuijadili hiyo dini ya kiislamu (mimi umenikosa).. Pili nadhani kama wema amekuwa mkweli katika kuzungumzia ukweli wa maisha yake huyo ni mtu mzuri, mungu hupenda watu wakweli na huchukia waongo na wanafiki..nataka nikurekebishe ..ivi kama wema anapata mwanaume na uyo mwanaume anamuahidi atamuoa then anamuacha unataka kusema ndio asidate mwanaume mwingine, kuchanika kwa mkeka sio mwisho wa hadithi ndugu yangu.. Hukumu ni juu ya mungu wewe huna haki ya kumuhukumu wema abrahamu sepetu, ni tabia chafu kujipotray kama wewe ndio malaika na kujidai kumwambia amrejee muumba wake unauhakika gani hayupo karibu na muumba wake??? Pia hii thread siku nyingine iweke katika jukwaa la chini hapo "celebrities forum" .
 

Muhimu ni ubinadamu wake ukienda zenj utashangaa watoto wa kiislam wanavyojiachia kiaina tena wengine ni wanaume na wengine magumegume na magubegube
 
Usiseme waislamu tu,kwani ninavyojua mimi hakuna maadili ya dini yoyote yanayoruhusu maisha ya namna hiyo.
 
nenda iraq (baghidad) uondoe ushamba .wanajiuza ndan ya burka [hijabu] pia jua kuwa eac zanzibar inaongoza kwa mateja pamoja na dini hii ilivyo na mafundisha mazur na makini,tumjadil wema na upuuz wake coz dini zote ni safi ila ss ndio tuna matatizo
 
Ninapata wasiwasi kama mmesoma Tenanzinyo na kumuelewa.

Kwa kifupi, amemshauri Wema kuacha kutumia kivuli cha 'mtoto wa kiislamu' bila kurekebisha matendo yake kwanza.

Ushauri huo ni mzuri, si kwa Wema tu bali wasanii wote wa filamu na muziki wa kizazi kipya ambao kusema kweli bila kupepesa macho wala kuuma maneno, wametawaliwa na kashfa mbalimbali za aibu kila kukicha.
 
Wanaume watano tu unakuja humu kulialia,kuna wengine hao watano ni kwa usiku mmoja tu,tena siku zote 365 za mwaka.
Kuna mashine hapa duniani,unacheza wewe.
 
Watu wengine bhana... tenanzinyo sasa ulitaka ajiite "mtoto wa Kikristo"? afadhali ya Wema kuliko hao wanaovaa mabaibui!
 

Nashukuru Mkosoaji kwa kunisaidia kuwaelekeza wadau wapatae muda wa kuisoma na kutafakari thread kabla ya kuchangia japokuwa kila mtu ana uhuru wa kuchangia kma jinsi anavyojisikia!
 
Last edited by a moderator:
Hebu muwacheni wema apumuweeeeeee jamaniiiiiii....... Kha!
 
badala ya sigda kutokea usoni, nadhani itakuwa imetokea kwenye "K"
 
''WEWE'' ndo unamfanya kuwa famous..Kuwa kama humuoni alaf 2one kama utackia tena story za huyo ''UBAYA''
 
Kwenye ishu ya kuchoma makanisa na kuiba sadaka mbona hukuweka gazeti lote hilo? au yenyewe inaruhusiwa na kolani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…