Wema wa Mayele ndiyo umemponza

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Nilifatilia kwa umakini sana uchezaji wa Mayele. Kila baada ya kufunga goli mara kadhaa alijivunja ili kumpa nafasi mkongo mwenzaje Makambo acheze.

Kuna mechi nyingi tu angeweza kufunga goli zaidi ya moja au hata kupata hatriki lakini tabia yake ya kujivunja ndo imemgharimu. Ni ngumu kuwa mfungaji bora kwa wastani wa kufunga goli moja moja.

Wema wake ndo uliomponza na anatakiwa ajilamu yeye mwenyewe.
 
Pia Nabi haweka kipaumbele jambo la kiatu hasa ukiangalia game hizo mbili za mwisho
Wewe mmebakiza mechi mbili ligi kuisha Unamuanzisha benchi Mayele kipindi chote cha kwanza?

Na ame ya mwisho Nabi alitamka kuwa kwake yeye kwanza ni yanga halafu ndiyo mtu
 
Kwa hiyo tuwasaidieje wana uto maana mna lia lia sana na striker wenu mwenye uwezo mdogo kukosa kiatu.

Kama ana uwezo mkubwa ieleze jamiiforum ana viatu vingapi kwenye kabati lake tangu aanze kucheza boli?
 
Nakubaliana nawe juu ya hili 100% zote.
Kama unakubaliana naye 100% basi amini wenzetu wakongo wako tofauti na Sisi. Labda niwafananishe na Wa Ivory. Hakuna Mtanzania anaweza cheza ligi ya SA akakaubali kumpisha Mtanzania mwenzake acheze. Nimemuona Mayele akifanyiwa Sub bila kulalamika lakini Hali haiko hivyo hata kwenye timu ya Taifa ya Tanzania. Mchezaji akifanyiwa Sub ananuna, kuna mmoja Mechi za mwisho mwisho wa ligi aliondoka kabisa kwenye benchi akaingia vyumba vya kuvalia.
 
Kwa hiyo tuwasaidieje wana uto maana mna lia lia sana na striker wenu mwenye uwezo mdogo kukosa kiatu. Kama ana uwezo mkubwa ieleze jamiiforum ana viatu vingapi kwenye kabati lake tangu aanze kucheza boli?
Na hizi ndizo akili halisi za mashabiki oya oya huko umbumbuni..!
 
Wanavvyomchukia mayele Hawa wachawi Hawa acha tu


Ila wachawi wenzao wakisema wanamsajiri hahahah utawaona wanamsifia mpaka kuramba viatu

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna hoja hapo idadi ya mechi alizocheza Mayele , ukifuatilia pia nafasi za wazi alizokosa utaona wazi kuwa angeweza kabisa kufunga zaidi ya goli 20! Hivyo tukubali tu kuwa uwezo wake ni mdogo na alichopata ndicho alichostahili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…