Huwezi kumfukuza mtu ambaye anaendana na matakwa ya waajiri wake.Kila kazi ina malengo yake na budget yake.Kwa sasa Wenger anaendana na budget ya Arsenal na malengo yao pia na ndio maana board inampenda na wala msitegemee kufukuzwa leo wala kesho labda kama timu itauzwa.Na timu ikiuzwa pia huyo mnunuzi kama atampa hela Wenger ya kununua timu ya kuleta kombe Wenger ana uwezo wa kufanya hivyo pia.
Kinachofanyika sasa hivi ni kuwa na timu yenye budget ndogo na inayoweza kushindana kitu ambacho Wenger kafanikiwa mpaka sasa na madeni yanalipwa vizuri tu na timu hela inaingiza vizuri.
Sisi mashabiki ndio tuna uchu mkubwa sana wa kombe kwani ndio mafanikio makubwa ya timu yoyote lakini wana board wao kombe ni sehemu ya lengo lao lakini sio muhimu sana, muhimu ni ku-balance kitabu cha mahesabu.N a kwa vile kitabu chao kinaenda vizuri chini ya uongozi wa Wenger kwamba anaipeleka timu kwenye nafasi nzuri japo kwa budget ndogo ndio maana hawatomfukuza.
Muhimu ni uvumilivu wakuu tutakula mbivu huko mbeleni.