Wenger aifikia rekodi ya Ferguson ya mechi 810 PL

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Leo katika mechi ya ugenini dhidi ya Crystal Palace , kikongwe Arsene Wenger atafikisha mechi ya 810 tangu aanze kuifundisha Arsenal kwenye Ligi kuu ya Uingereza , hii ni rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Alex Ferguson aliyekuwa kocha wa Man U.

Kila la heri Wenger .
 
Reactions: BAK
Abwage manyanga sasa. Kishachokwa na wapenzi wengi hata wachezaji. Wengine wanatamani sana kutinga kwenye jezi za Gunners lakini Babu hawamtaki awepo kama Kocha.

Vipi kwa idadi hiyo ya mechi hizo ana mafanikio sawa na Ferguson?
 
Abwage manyanga sasa. Kishachokwa na wapenzi wengi hata wachezaji. Wengine wanatamani sana kutinga kwenye jezi za Gunners lakini Babu hawamtaki awepo kama Kocha.
KWELI KAKA ME MWENYEWE GUNNERS ILA WENGER NO!!!!!!!!
 
Yet, kashinda ubingwa wa EPL mara tatu tu, aachie ngazi tu.
 
Hii ni rekodi ya PL tu iliyoanza 1992 na haihusishi meshi za SAF kato ya 1986 na 1992 za First division.

SAF: 1992 mpaka 2013 misimu 21
AW: 1996 mpaka 2017 misimu 21
 
Fafanua kidogo mkuu

Ferguson alianza kazi 1986 mpaka 2013 ambayo ni misimu 27. Kati ya hiyo misimu 6 ilikuwa wakati wa First division na misimu 21 ikiwa ya Premier league ambayo ilianza 1992.

Sijui unataka nifafanue nini tena?
 
Si ndio umefafanua kama hivi mkuu .
 
kuhusu vikombe..usimlinganishe Wenger na ferguson..kuanzia 2004-14 ..arsenal ilikua na kazi ya kulipa deni LA uwanja hivyo kushindwa kushindana kwenye soko LA wachezaji..ndiyo maana Ferguson anataka watu wamuheshimu Wenger kwa kazi aliyofanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…