Wenger awataka mashabiki kudumisha imani baada ya kichapo cha Anfield

BIGstallion

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
6,324
Reaction score
7,913
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa na imani baada ya kile alichosema kuwa ni uchezaji wa kusikitisha sana baada ya klabu hiyo kucharazwa na Liverpool 4-0 katika mechi ya Ligi ya Premia Jumapili.

Gunners hawakuwa na kombora hata moja lililolenga goli baada ya uchezaji mbaya ambao ulikosolewa pakubwa na mashabiki na wachanganuzi wa masuala ya soka.

"Iwapo baadhi ya watu wanahisi kwamba mimi ndiye tatizo, basi naomba radhi kwamba mimi ndiye tatizo," Wenger aliambia Sky Sports.

"Lakini tunataka mashabiki wetu waendelee kuwa nasi hata baada ya uchezaji mbaya hivyo na kushindwa."
Aliongeza: "Jambo pekee ambalo tunaweza kufanya ni kurejea na kucheza vyema."

Wenger alitia saini mkataba wa miaka miwili mwishoni mwa msimu uliopita, licha ya baadhi ya mashabiki kumtaka aondoke. Klabu hiyo ilimaliza nafasi ya tano ligini msimu uliopita na kumaliza nje ya nafasi za kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 21 ambayo wamekuwa na Wenger.

Hata hivyo, walifanikiwa kushinda Kombe la FA.
Wenger alimwacha mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingine na klabu hiyo Alexandre Lacazette kwenye benchi wakati wa mechi hiyo Anfield, lakini alimchezesha Alexis Sanchez kwenye kikosi cha kuanza mechi mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu. Hata hivyo, vijana wake walipanguliwa na mabao kutoka kwa Roberto Firmino, Sadio Mane, Mohamed Salah na Daniel Sturridge.

Alipoulizwa nini kilikuwa kibaya na uchezaji wa vijana wake, Wenger alisema "kila kitu".

"Hatukuwa katika kiwango kifaacho tangu dakika ya kwanza - kimwili, kiufundi na kiakili - na tuliadhibiwa," alisema Mfaransa huyo.

"Uchezaji wetu leo haukubaliki. Ni kweli kwamba leo tulikuwa wapinzani wepesi kwa Liverpool".

"Uchezaji wetu ulikuwa mbaya mno. Sitaki kutekwa na hisia, lakini tuna safari ndefu, na kuna sababu zinazosababisha hilo, na wachezaji sasa wanaelekea kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa, lakini lazima tujifunze kutokana na uchezaji wetu leo."

Chanzo:BBC
 
Hii timu ukiiangalia kuanzia mechi ya kwanza ya msimu imekuwa inakatisha tamaa sio arsenal ya ushindani au ambayo timu pinzani inaweza kuihofia kutokana na uchezaji wake.
Hivi mtu kama danny welback anafanya nn kwenye timu huku kwa Wenger ndo kila kitu beki inabadilishwa kila mech imefikia hatua wenga anafanya majaribio ya wachezaji kwa timu kubwa kama Liverpool Leo hii unamchukua beki wa kulia unampeleka acheze kushoto kwa Mara ya kwanza tena na Liverpool halafu Wenger analaum team kuwa haijacheza vizuri!!!mjinga xna huyu babu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseee inauma saa kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah ukipata mke kama mashabiki na wamiliki wa Arsenal hakika hutakufa mapema
 
Tumheshimu Arsene Wenger kwa sababu nina kila sababu ya kuamini kwamba kila mpenzi wa Arsenal ameanzia na mafanikio ya Wenger. Ni wachache wanaoweza kujua kabla ya Wenger alikuwepo nani na alikuwa na mafanikio gani.

Hata kama unaona humhitaji mwambie kwa lugha ya staha na siyo kutukana kama huna wazazi bwana. ebooo
huyo ndo aliyekufanya ukaipenda arsenal na mapambio ushamwimbia sana, alaaa...heshima ifate mkondo wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…