Wenger hali ni tete na top four race

Wenger hali ni tete na top four race

Joined
Dec 28, 2016
Posts
50
Reaction score
52
Akili, mwili na mtizamo hufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano ili kufanikisha jambo flani... akili na mtizamo vikiwa katika hali mbaya basi hata mwili utashindwa kutuonyesha kilicho bora, Ndivyo ilivyo kwa Arsenal, wachezaji wamechoka akili na wamekata tamaa, wana mtizamo negative na kocha wao Wenger, hawana morale yoyote... kila mchezaji anacheza chini ya kiwango... hawajaona mafanikio ya uwepo wake... nafikiri zile heavy defeats from Bayer Munich kwenye champions League ndio zimesababisha psychological damage kwenye performance yao

Kwa sasa kumaliza top four inaonekana kama Mlima mrefu kwao, wakati Liverpool Manchester City, Manchester United zote zinashinda alafu yeye anapoteza tena kwa kipigo kikali toka kwa Crystal Palace, hali ni ngumu sana... kuna mechi za Arsenal vs Manchester United na vs Tottenham, kwa hali ya wachezaji kwa sasa itakuwa ngumu sana kwao kupata matokeo

Bado fixtures zilizobaki zinawabeba Liverpool na Manchester City katika kufuzu UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao.. Manchester United ana fixtures ngumu sana ambazo ndio zinaweza kuwa kikwazo katika kuingia top four

Manchester United vs Manchester City, Chelsea, Arsenal, Tottenham... ni ngumu sana kwa Manchester United kufuzu UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa kupitia nafasi ya nne kama ilivyo ngumu kwa ngamia kupenya kwenye tundu la Sindano

CRYSTAL PALACE 3-0 ARSENAL THE GUNNERS, WENGER OUT

POINTS MKONONI NI BORA KULIKO MECHI MKONONI
 
Back
Top Bottom