Wengi wamenufaika na msiba wa Kanumba

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
13,786
Reaction score
2,095
Ndugu marafiki na maadui
Kuna watu wengi wamenufaika sana na huu msiba wa Kanumba.
Nianze na hawa wana Kamati ya mazishi tusubiri uchakachuzi mkubwa wa mapato yatokanayo na rambi rambi ya msiba wa Kanumba na mwishowe wafiwa wataachwa watupu bila kifuta jacho maana itapigwa hesabu hizo balaa itaonyesha kilicho patikana kimetumika choote na wengine kutoa pesa zao mfukoni.
Wauza maji, mihogo, ndizi, karanga, sigara n.k hawa jamaa wamepiga sana bao msiba huu wa Kanumba
Vibaka hawa jamaa nao hawakuwa nyuma watu wamelizwa viatu, mikoba, simu, fedha yaani ni maumivu kila mwombolezaji alikuwa ananung'unika kivyake vyake rohoni. Vibaka wamepiga sana dili msiba wa Kanumba
Waokota chupa hawa nao jana wamenufaika sana kwa kujaza mifuko na mifuko ya chupa za maji wamepiga sana dili.
Wakodisha magari hao jamaa nao wamepiga sana dili watu walikuwa wanakodi magari ya kifahari wakauze sura msibani kwa Kanumba.
Boda boda /Bajaj hawa jamaa nao Mungu aliwaona maana wamepiga sana kazi ya kuwatoa waombolezaji toka sehemu moja na kuelekea sehemu ingine Mungu aliwaona nao.

====================================
umesahau wachapishaji tishet banners. Etc hawa ndio walipiga hela kuliko

TV na redio zilipata vipindi vya kuweka, magazeti pia yalipata dili, hadi jamiiforums na internet nazo

Hata Blogs za watu mbali mbali zimevunja records ya kutembelewa na watu
 
we ulitaka watu wale wapi ? kufa kufaana.
 
Nianze na hawa wana Kamati ya mazishi tusubiri uchakachuzi mkubwa wa mapato yatokanayo na rambi rambi ya msiba wa Kanumba....

:suspicious: Hatuwezi kufika pahala tukawa na mwelekeo kuwa inawezekana kukawa na 'kamati' aminifu?
 
umesahau wachapishaji tishet banners. Etc hawa ndio walipiga hela kuliko
 
TV na redio zilipata vipindi vya kuweka, magazeti pia yalipata dili, hadi jamiiforums na internet nazo
 
we ulitaka watu wale wapi ? kufa kufaana.

Kweli mkuu ndo maana watu huwa wanang'ang'ania kuingia kwenye kamati wengine wanahonga kabisa
 
Mh jamani zote ni sadaka kwa ajili ya marehemu

R.I.P the great Kanumba
 
wote tisa. Kumi ruge mutahaba. Huyu kanufaika kuliko wote. Ukizingatia kanumba hakua na ndugu yeyote mzito. Msiba wote ulikua chini ya wana kamati!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…