"Wengi Wape"...Uamuzi Mzito

umuhimu wa kwanza ni...


  • Total voters
    40

....Keren_Happuch wala hujakosea, ndio maana nikajisemea niwaulize nyie wenzangu kwa experiences zenu ila,
issue hii kidogo ni tofauti na 'shule' iwe ni college, au university ambayo ni short term, iwe ni 6mths, 1yr au 3yrs...

...kazi kidogo ni tofauti, kwani inaweza ikawa ni 5yrs- 10yrs contract, ....au kama ndio 'maboksi,' miaka 15 sasa kuna watu hawajarudi makwao, ...wazee, ndugu jamaa na marafiki, wanaoa, wanaugua na wanaokufa wao wanatuma pesa tu za shughuli...!
 
kipato na familia vyote vinategemeana, ila kipato ni muhimu zaidi manake kitaiwezesha familia kuwa bora, kuwa mbali na familia haimaanishi kuwa umeacha kuijali, makubaliano ndicho kitu cha muhimu hapa.
 

Mhhh...sasa hapo kwa muda mrefu kiasi hicho, basi inakuwa ngumu kweli! Mimi nafikiri pia cha muhimu, familia ina mipango gani? Sasa kweli MBU...15 yrs away from your family???!!! Hapana jamani...sasa hapo si ndo unakaribisha majaribu mengine, halfu unamsingizia shetani! Lakini iwepo mipango ya familia!
 

...lol...hiyo red nimeipenda.

Umefafanua vizuri sana, lakini ombi la option ya tatu siikubali, ndio maana nikasema wengi wape, na kwenye 'sandakarawe' kuna kupata na mmoja anakosa..he-he!
:eyebrows:

unakaa nao mbali sababu tu ya kuhakikisha they are getting the best in this world

...kuna mahala nimewahi soma "...money is not everything!"
...hii nayo unaizungumziaje kwenye mdahalo huu?
 
kipato na familia vyote vinategemeana, ila kipato ni muhimu zaidi manake kitaiwezesha familia kuwa bora, kuwa mbali na familia haimaanishi kuwa umeacha kuijali, makubaliano ndicho kitu cha muhimu hapa.

...sweetlady karibu na asante kwa mchango wako, umegusia makubaliano... nadhani hii inahusisha zaidi baina ya mke na mume. Je? nini athari za makubaliano haya kwa mtoto au watoto ambao kwa kipindi kirefu wataishi bila baba/mama? ...ushawahi lifikiria hilo?

...."the precious time lost, is lost forever!"



...haya basi nisikuchanganye na 'wabeba maboksi' ili upate kunisaidia.
Lets stick kwa hii issue yangu (inayonifanya niwe mbali na familia
kwa zaidi ya miezi sita mpaka nane kwa mwaka
)...huu mwaka wa kumi na mbili sasa...:yawn:
 
Mzee mosquito hiyo kazi ni kwa ajili ya welfare ya familia yako as well

I had a relative alikuwa na dilema of ur sort yeye alipiga mgodini but as soon as alipomaliza mjengo wake pale A town aliquit job na kurejea home kwa familia yake na sasa they are happy kwa sanaa tu. Hapo u must strike a fine ballance ili familiymembers waone faida ya wewe kuwa mbali nao.....comparative advantage......

Set the target and hit the bull.......kabhaaaang u get up and slowly u re-join ur family........sio ukae wee mbali na ukija huko ni story tu na kuchukua tena na kidogo ulichokuta hapo home unatokomea tena

Pole kaka mzani huo ballancing point yake ni ngumu ila inatafutika.....no formula though
 

...safi sana,...

...kuishi kwa malengo muhimu, ...jamaa yako alipata 'jiwe' likamlipa kutimiza malengo & majukumu yake.
Ila majukumu yanaendelea kila kukicha bana, na watoto wanapokua, ...gharama za pampers na cerelac
zinaondoka na kufidiwa na gharama za Shule za Academy, kisha kusaidia kulipia vyuo vikuu...mamilioni hayo!

...na hii recession, hata biashara za kusaidia kulipia LUKU pia inakuwa issue...
Tunarudi pale kwenye issue ya kuendelea kutafuta kwa nguvu zote huku nikiweka rehani mahusiano
na familia....
"...asiyekuwapo na lake halipo!"
 

For this specific case uliyoileza hapa juu, familia inahusika sana. binafsi natafuta Pesa ili niweze kufurahi na familia yangu siyo vinginevyo. Kukaa mbali na familia na ukawa na pesa YANAWEZA kuleta hali ya kuishi maisha ya kihuni yasiyo na maana wala heshima na kujikuta kipato chako kinaishia kwa machangudoa na wasiousika, kuna faida gani hapo?
 
Reactions: Mbu
Vyote ni muhimu, unaweza kujikuta unakimbiza kipato ukapoteza familia uliyokua unadai ndio unayoisumbukia, unaweza ukakumbatia familia huku mkiwa na matatizo mengi ambayo yangetatulika iwapo ungekimbizana na kipato.

Kwahiyo ningeshauri utafute balance, usikipe kipato 70% na familia 30% kwasababu waweza jikuta umetupwa nje ya mzani. Angalia huko unakofuata hicho kipato, angalia je hicho kipato/muda/umbali vitaruhusu wewe kuwa karibu na familia kiasi cha kutosha? Jiulize, je familia yako inaweza ikasurvive kwa kupata pesa nyingi bila baba around? Je mnaweza mkasurvive bila hizo pesa huku baba akiwepo karibu? . . .
 

Bless you Lizzy,....woww!
 

Tukija kwenye swala la watoto hapo sasa tunahama kwenye kipengele cha makubaliano na kuhamia kwenye kipengele kingine cha malengo. Ni vizuri sana watoto wakapata malezi ya baba na mama, hiyo ni haki yao ya msingi kabisa....ndio mana hapo nimesema inabidi kuwa na malengo madhubuti, manake mke na mume mnaweza kufanya makubaliano lakini wakati huo huo yakawa na madhara kwa watoto japo pia yanaweza yasionekane kwa wakati huo... Mbu kila kitu kwenye haya maisha ni kwa mipango na malengo... Lazima ujipange na kuhakikisha kuwa huegemei upande mmoja sana( kazi iwe 50% na familia iwe 50%)...familia hata ikiwa na kipato kiasi gani amini usiamini kama haiko pamoja( baba, mama, na watoto) haitakuwa na furaha...japo kwa nje inaweza kuonekana yenye furaha... Mada yako ngumu bana, naungana na AshaDii kudai kipengele cha both...
 

...umenifunga tena kwenye jibu,....hapo una maanisha familia kwanza kabla ya kipato, si ndio?
Asante, ni maamuzi magumu yanayohitaji hekima.

Hapana sijakufunga Mbu, labda sikukamilisha usemi "Dereva mzuri ni yule anaye chunga usalama wake na abiria wake" usalama wenu wote unategemea kipato vinginevyo ndo mwanzo wakusemwa una nini watoto wanasoma kayumba mpaka sasa, sijui tutaendelea kupanga mpaka lini, mara ohoo nimechoka kubadilishana joto kwenye daladala, nk. Kafanye kazi kama mke ni muelewa atakuogezea busara aliyojaliwa ktk muda mtakaokuwa mbalimbali kwa muda.
 
Reactions: Mbu

...hahahaha, sasa hapo kwenye wekundu nawe umenifunga, maana umeanza vizuri tu kuwa malezi ya watoto yanahitaji presence ya wazazi wawili....sasa ugumu upo wapi namai nachotaka ni uamuzi kipi bora kati ya kipato kikubwa au familia?


Ahsante Mbu. . . nawe pia.

Hopefully umekaribia kupata muafaka.


...unajua kama ni mtumbwi, wangu ulikuwa anaingiza maji. Angalau umenitupa kifuniko cha X-pel kunisaidia
kuyapunguza...

kiukweli,...kuna kitu umegusia kuhusu balancing hapo...yaani umenipa mwanga wa ku sacrifice kipato kinachokidhi 95% ya mahitaji ya familia, ili kuweza kupunguza hilo gap la umbali....

...au nimekuelewa vibaya? wengine mnasemaje! :A S-coffee:
 

...hahahaha, sasa hapo kwenye wekundu nawe umenifunga, maana umeanza vizuri tu kuwa malezi ya watoto yanahitaji presence ya wazazi wawili....sasa ugumu upo wapi namai nachotaka ni uamuzi kipi bora kati ya kipato kikubwa au familia?

Vyote bora ila kwa kiasi, usiegemee kwenye kipato ukasahau familia, wakati huo huo pia usiegemee zaidi familia ukasahau kuwa watakiwa kuwa na kipato kwaajili ya familia. Mbu mie naona vyote ni bora ila kwa kiasi... Vinategemeana sana hivyo ni kazi yetu sisi kuhakikisha kuwa tunabalance!
 
Reactions: Mbu
pesa hujenga familia yoyote uitakayo kuanzia ya malaika hadi ya mashetani, ya muda mrefu hadi mfupi... lakini familia bila pesa ni nyumba ya ujinga, umaskini na maradhi
 
Reactions: Mbu

Umenipata sawia Mbu, usishikiliee sana kimoja na kusahau kingine maana mwisho wa siku unaweza ukapoteza familia ukashindwa kuelewa hata ulichokua unahangaikia. Chukua karatasi na kalamu, piga hesabu ya umbali, piga hesabu ya mshahara (utatosha kuwaweka karibu, au ni chakula/malazi na mavazi tu), piga hesabu ya muda mtakaokua apart (is it reasonable? Sio unakua mbalia kiasi kwamba ukirudi unakuta watoto walishaota ndevu wakati uliwaacha bado wanaendesha baiskeli za mbao).
Unaweza ukaandika list mbili. . . KAZI (faida na hasara), FAMILIA (faida na hasara) alafu upime uzito.
 
Reactions: Mbu

...ngoma ipo kwenye kujishusha bana....imagine maisha yote umepigania kufa na kupona kuipanda ngazi hiyo ushafika kileleni unagundua kuna priorities nyingine inabidi uzi sacrifice...

...bado nacheza 'sandakarawe' nini zaidi kazi yenye kipato kizuri vs familia...
 
kwa maisha yalivyo magumu kwasasa, riziki ni popote, makubaliano ni ki2 muhimu sana ktk ishuz kama hizi, c shughuli ndogo but ikileta mafanikio ni kheri 2pu...niliwahi kubaki na familia kwa mwaka na nusu but kwa makubaliano magumu haswaa, nilikuja kuona faida yake alipomaliza huo muda, japo niliteseka but wanasema mvumilivu huwa mbivu......
 
Mbu & The Boss,

Naomba mnisaidie kidogo....Which of the two is more romantic??

Babu DC!!!
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…