Pre GE2025 Wenje abanwa tuhuma alizozitoa kuhusu fedha za 'Join the Chain', apata kigugumizi ghafla

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Ezekia Wenje ameulizwa kuhusu takwimu za madai ya ubadhilifu wa fedha za mkakati wa 'Join the Chain' ambazo alizitoa katika mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita.

Akijibu swali hilo, Wenje amesema aliainisha yaliyofanyika nyuma ya pazia na sio kutoa takwimu kama muuliza swali alivyosema.

Soma: Ezekiel Wenje: Kuhusu zilipoenda pesa za Join The Chain muulizeni Godbless Lema. Yeye ndo alikuwa Mwenyekiti!

Wenje amesema hayo Jumanne Januari 21, 2025 akiomba kura katika uchaguzi wa chama hicho unaofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ni 'Nguvu ya umma'

Msingi wa hoja hiyo ni baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika kulitolea ufafanuzi suala hilo lililoibuliwa na Wenje wiki iliyopita, akidai mkakati huo ulikuwa wa kumpindua Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Pia, Soma: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?
 
View attachment 3209390
Pia, Soma: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA nafasi ya Mwenyekiti & Makamu Mwenyekiti 2025: Ni Mbowe au Lissu?
amejibu vizur, kwa ufasaha na kisayansi sana,

wenye majibu yao mfukoni wakabaki kubababika na kukodoa macho tu dah, siasa ni sanaa 🐒
 
Back
Top Bottom