Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Baba akuwa mkali kwakweli. sijui nilipokuwa Mdogo ilantangu nilipopata Akili sikumbuki Kama alishawahi kunyanyua mkono wake kunipiga, Ila mtiti kwa bi mkubwa ni balaa.

Ilikuwa inafika kipindi ukichezea bakora kwa mama Baba anagombelezea Apumzike kwa amani.
 
Mshua alinichapaga viboko mbele ya demu wangu alikuja kusuka.
Dingi amekuja mchana kula chakula akakuta hakuna maji hata ya kunawa mikono, kubabake alinichapa sticki hizo.
Demu wangu alikua nje anasukwa na dada yangu, dingi ananichapia sebuleni.
Kwa kuwa nilikua sitaki demu wangu ajue kama nachapwa, nikawa najikaza sipigi kelele.
Dingi akajua viboko havini umizi, akaanza kunipiga na mavibao, kubabake nilivimbaga mikononi.
Mara Paaaap nikatoka na mindoo kwenda kuchota maji, mialama ya viboko kwenye matako, mgongoni, mikononi.
2001 hiyo Kiloleni Tabora
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Madingi wakali dawa yao wapelekee wajukuu tu sasa hivi wanavyozeeka uone.
true yaan wanavyopelekwesha hadi unajiuliza hivi ndo yule Dingi yangu bandidu ninayemjua mimi au
mana wanakuwa wa pole kupita viwango mbaya zaidi anafanyiwa vitu ambavyo wewe mwenyewe mwenye mtoto kimfanyia usingeweza wanawadekeza zaidi ya maraika
yaan utasikia tu acha nitakuchapa
kama kuna kiti chake cha uzee hakai mtu lkn huyo mjukuu wake anapanda na michanga tena wakati mwingne wanabanana hapo kukaa kiti kimoja
station ya tv anachagua yeye
wkt enzi nzake thubutuuuu uweke station unayotaka wewe wakati yeye yupo kwanza utaanzaje
 
Dah mdau kumbe wewe niwanyumbani kabisa tabora
 
Mimi nakumbuka siku ya mwisho dingi kunichapa.....alinikuta nasoma saa sita usiku yeye yuko nzwiiiii......akaniuliza kwa nini sijalala, nikamjibu huoni nafanya nini.....akajaa povu....akafuata fimbo kwani alikuwa anaziweka sehemu......akaanza kunitandika......nilitulia tuu, ila ikafika wakati nikasema leo lazima nimuonyeshe huyu mzee......niliikamata ile fimbo na nikaivunja vipandevipande.....kulikuwa na music system ya Phillips niliifuata na nikaivunja vipande vipande.......nikaenda kwenye kabati la vyombo....nililiangusha na almost vyombo vyote vya udongo vilivunjika.......ndio ilikuwa mwisho wa mzee kunichapa......
 
Madingi zenu walikuwa madikteta maana sio fimbo hizo


Swissme
 
Madingi wanaokubali kupelekewa wajukuu hao si wakali, wale wababe wa vita mjukuu akija asalimie na kusepa, hawana muda wa kulea mtoto na mjukuu!
 
hahaha.... kwahyo dingi angu ndio muasisi
 
We mhenga 99 nlikuwa nna miaka mitano
 
Duh noma
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimechekaaa...kujifanya mkarimu kuliko mwenye simu yake ndio nini sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…