Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Ngoja nami niandike mambo kadhaa ambayo yamenifanya niamini hakuna mzee kama mzee wangu.

1. Siku moja tumeenda kwenye ngoma masikini nikaongozana na dada zangu kwenda huko mzee alikuwa yupo safarini akarudi akakuta milango yote imefungwa na kuku wapo nje yaani full tafrani hapo nje, wazee wa ngoma tukaingia kwa mbwembwe shikamoo baba!!! Hahahha tukafungua mlango kuku wakaingia ndani msosi ukapikwa na watu wakala.

Dingi yupo kimya tu anasoma mchezo nikamaliza kula nikawa naenda kulala kidume nikaitwa njoo hapa unaenda wapi nikamjibu kulala akasema toa godoro lako likunje, nikakunja godoro vizuri nikamaliza akasema liweke chumbani kwangu nikapeleka chumbani godoro haya nenda ulale. Bwana wee Kitanda cha chuma hakina kitu nikafika kidume nikalala kwenye vyuma kwa usimamizi wake hadi majira ya saa 8 hivi nagalagala kwenye vyuma, ngozi imeweka alama kama nimechapwa bakora aiseeee. Wale dada zangu wenyewe walifungwa juu ya kenchi usiku kucha hadi asubuhi, Asubuhi niliamka poa tu nikakanda mwili vizuri nikaendelea na majukumu ya utoto.

2.Kuna mdogo wangu alikatwa masikio.

3.Vikojozi walikuwa wanalala kwenye mfuko, wanaingizwa humo usiku kucha watatolewa asubuhi.

Hakuna kusema neno NITAKUPIGA hata kama ni kwa mdogo wako akisikia hilo neno ni kipigo Heavy kwa aliyesema "alikuwa anadai yeye ndiye mwenye uwezo wa kupiga kwenye ule mji".

Ukizira kula jiandae kula kwa lazima na chumvi ikizidishwa maradufu kwenye mboga chini ya usimamizi wake.

Kuchomwa kwa mvuke ilikuwa kawaida sana kwetu.

Ukipigwa haja kubwa isitoke shukuru Mungu kipigo cha siku hiyo.

Aliwahi kukunja mzazi mmoja ngumi hadi kwenda polisi (ila hiii sisemi).

Nilikuwa nafata maji usiku saa mbili kisimani ambapo ni zaidi ya km 2 pekee yangu nikiwa under 10 years.

Nipo safarini nikifika nitawaambia watu wa Tanga nipokeeni hapo stand. Nipo kwenye basi la Simba Mtoto natokea Isamembwe.
 
Wazazi wengi walikua makatili nyie lo,,basi kila mtu anashindana kuonesha mzee wake alivyo katili hahaha
 
Mzee wako alikua abuse sana,wazee kama hao wakishakua wakubwa wanakua wanahitaji kweli mapenzi ya watoto wao lakini utakuta watoto wanamchukulia poa tu.
 
Duh, huyo jamaa yako yuko wapi sasa hivi? Mzazi kuwa mkali kupita kiasi siyo malezi yanayofaa! Kitakachotokea ni chuki/upendo wa mtoto kwa mzazi kutokuwepo!
 
[emoji115] [emoji119] [emoji119] [emoji119]
 
Hongeran kuwa na madingi, wengine kama sisi hatujafanikiwa kuwaona ni hadithi tunazosimuliwa
 
[emoji1][emoji1][emoji23][emoji23][emoji23]mkuu huyu mzee bado yupo hai kwelii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…