Wenye maduka jihadharini na watangazaji wa tv!

Amina Thomas

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2008
Posts
272
Reaction score
130
Napenda kutoa tahadhari kwa wenye maduka hasa ya urembo. Jihadharini sana na kuwaamini baadhi ya watangazaji wa tv na redio hasa wa kike. Watu hawa wanapenda sana kukuzoea na kujenga uaminifu halafu wanakimbia na madeni. Watu hawa kwa umaarufu wao wanapenda maisha ya juu wakati kiukweli uwezo huo hawana. Mimi yamenikuta lakini baada ya kufanya uchunguzi nimegundua kua hata wengine wengi tu wamefanyiwa hivyo. Wakitapeli duka moja wanahamia lingine. Tabia hizi sio nzuri kwa kua tukiamua kuwaanika itakua aibu
 


wewe unawaheshimu wezi naona
ukiwataja hapa kuna shida gani?
 
Amina Designs??

Anyway, Kama wameweka ushikaji pembeni na kukuibia, nawe weka ushikaji pembeni na kuwataja.

Wakimwaga mboga,.....!!!
 
Kwa nini usimtaje mwizi wako??kwa nini umuogope??? Kama hutaki kum taja live tutamuepuka vipi?au unawapakazia wbndishi?thibitisha kauli zako.
 
... Hana Lolote Huyu. Mbona ameambiwa awataje ameingia mitini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…