Wenye Maduka ya Biashara na Watumiaji Wengine - Nahitaji Mawazo Yenu

Tatu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2006
Posts
1,143
Reaction score
372
Habari za leo wananchi.

Nina wazo la ku-develop website ambayo inaweza kuwa ya msaada kwa wenye maduka ya biashara na watumiaji wa nyumbani. Kabla sijafanya hivyo, inabidi nifanye homework kidogo nione je kama kunahitajika huduma hiyo ya website au la kuliko kupoteza muda wangu.

Najua kuna watu wengi wanaenda China na Uarabuni kununua vitu vya biashara na vya nyumbani. Lakini pia kuna Watanzania wengi wanaishi nje na hurudi nyumbani mara kwa mara.

Idea ni kwamba, niandike website ambayo inawawezesha wafanya biashara na watumiaji wa vitu mbalimbali kubandika mahitaji yao halafu watu walioko nje ya nchi (Marekani, UK, nk.) waka-bid na ku-initiate mawasiliano na mfanya biashara/mtumiaji husika ili wakati wanarudi nyumbani wavilete baada ya makubaliano.

Je wewe kama mfanya biashara au mtumiaji wa nyumbani, unafikiri website ya namna hii inahitajika? Itakuwa na manufaa yeyote kwako?

Tujadiliane kwa umakini na uchambuzi yakinifu.

Thanks
 
Ni wazo zuri, wasiwasi wangu ni namna utakavyo-control kuhakikisha hakuna utapeli kupitia website yako. Kwa wenzetu ambako kuna sheria tight na zinafanya kazi, wazo kama hili lingewezekana, ila kibongobongo mmhh nina mashaka!
 
Nashukuru kwa mchango wako na ni suala la kuliangalia kwa makini. Kwa sasa, zaidi itakuwa ni mawasiliano na makubaliano yao zaidi. Kwa hiyo inabidi kila upande ujiridhishe kabla ya makubaliano yeyote. Pia wanaweza kuandikiana mikataba ili wawe na ushahidi.

Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…