Mzukulu
JF-Expert Member
- Feb 14, 2020
- 1,401
- 2,641
Kuna Tangazo la Redioni nalisikia karibu katika Redio zote Kubwa nchini ambalo linatoka katika Mamlaka husika linasema kuwa Uvaaji wa Barakoa ( Masks ) ni kwale Walioathirika tu na Maambukizi ya COVID-19 na Wanaowahudumia na si kwa Watu wengine na kwamba wakifanya hivyo watakuwa wanajihatarishia Afya zao.
Hapo hapo tena tokea Juzi nimenza Kusikia Matamko kutoka kwa Watu wenye Dhamana za Kiuongozi ( Serikalini ) zikiwahimiza na kuwataka tena kwa Kuwalazimisha kabisa Watanzania kuwa wanatakiwa sasa Kuvaa hizo Barakoa ( Masks ) ili wajikinga na COVID-19. Na nimeona Mitandaoni na hata Kusikia na Kuona Runingani wengine wakitishiwa kuwa wasipozivaa basi watashtakiwa.
Tafadhali kama Watu ( Wakubwa ) wa Serikalini wapo hapa JamiiForums watusaidie kutuambia lipi ni Jambo sahihi na ni nani kwa sasa Sisi Watanzania tunapaswa tumsikilize kati ya Mtaalam wa Afya anayezuia Uvaaji wa Barakoa kwa asiyeathirika au Mwanasiasa anayetulazimisha tusivae ili tusife?