herio
JF-Expert Member
- Jan 1, 2021
- 2,245
- 4,320
Wasalam wana JF
Mimi ni kijana najishughulisha na ujasiriamali kwa kufanya biashara ya duka la rejareja pamoja na shughuli zingine. Dhumuni la kuleta uzi huu ni kutokana na kuyasoma mazingira haya ninayofanyia shughuli zangu na kuona fursa mbalimbali zinazohitaji mitaji midogo pamoja na mitaji mikubwa. Kwa leo nitaenda kuwafafanulia mawazo mawili ya biashara nilioyaona yanalipa kwenye eneo hili nilipo halafu tutajadiliana kwa pamoja.
1. Duka la jumla (wholesale)
Wazee kama nilivyowaambia hapo juu kwamba najishughulisha na biashara ya duka la rejareja la bidhaa za nyumbani kwa wanaofanya biashara hiyo watakuwa wanaelewa kwamba huwa bidhaa tunachukulia kwa wafanyabishara wakubwa wa maduka ya jumla. Kwa hii sehemu niliopo sio mjini lakini hii biashara inalipa sana wakuu kwa sababu zifuatazo:
i) Wafanyabishara wadogowadogo wote tunaenda kufunga mzigo mbali na hapa yaani kama km 5 pia sehemu nyingine mpaka km 15
ii) Hii sehemu ipo katikati ya vijiji kadhaa ambavyo vina maduka ya rejareja na zote zinahitaji bidhaa
iii) Hii sehemu ipo karibu na makao makuu ya mkoa yaani ni kilomita kadhaa tu kwa maana ya kwamba wewe muuzaji wa jumla hautachukua umbali mrefu kuchukua bidhaa zako.
Naam wakuu ngoja sasa niwaambie bidhaa utakazouza kwa jumla na zinatoka haraka kwa eneo hili
Sukari,unga wa ngano,sabuni za unga na vipande(bidhaa hizi unaweza ukaenda kufungia kiwandani moja kwa moja kwa bei nzuri) Mafuta ya mgando aina zote kwa ujazo tofauti tofauti, Soda za chupa za pepsi na koka(hizi unaletewa moja kwa moja dukani kwako hautapata gharama yoyote kufuata)
Soda za plaskiti za mo, jambo, azam, coca na pepsi pia utaletewa moja kwa moja dukani kwako
Maji kuanzia ujazo wa nusu,lita nk pia utaletewa moja kwa moja dukani
Nafaka kama mchele na karanga pia za utauza kwa jumla vilevile
Mbali na hizo utaleta na bidhaa zingine kwa uchache tu ila hizo hapo juu ni za muhimu zaidi
Wakuu kwa mahesabu yangu binafsi nimeona mtaji wa millioni 100 unatosha kabisa kufanya biashara hii ingawa kwa kuanzia milion 50 pia sio mbaya..maelezo mengine nitayatoa kwenye comment
2. Petrol & diesel station
Wakuu sina maelezo ya kujitosheza kuhusu biashara hii lakini hii sehemu ipo vizuri kwa hii biashara..
Pikipiki zipo za kutosha sana zile za wenyeji pamoja na wapita njia pia kuna barabara kubwa inayoenda mkoani na mabasi yanapita kila siku. Wakazi wa huku pia wanafanya kilimo cha umwagiliaji wakati wa kiangazi kwa kutumia majenereta ambayo yanatumia petroli msimu wa kiangazi kuanzia mwezi wa 5 mpaka 11
Kwa wenye mitaji naomba muangalie mawazo hayo mawili hapo juu ingawa mimi naona wazo la kwanza ndio lina hela tena nyingi sana
Karibuni kwa mjadala pamoja na maswali
Nawasilisha.