Wenye nchi na wananchi, Taifa kubwa na Umoja wa Mataifa

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Huwa nasema timu za Kariakoo ni Kulwa na Doto na àmbao tulishafanikiwa kuvuka mitego ya siasa zake tuna Amani zaidi.

Miaka ya 1990 Simba walikuja na Nick name ya Simba TAIFA KUBWA na ikahit vibaya. Kaulimbiu ya TAIFA KUBWA iliwabeba Simba ndani na. nje ya nchi maana ni kipindi hiki walifika fainali ya Kombe la shirikisho na kukosa ubingwa chupu chupu mbele ya Stella Abidjan ya Ivory Coast wakiwa chini ya udhamini wa Mzee Azim Dewji. Pacha wake alipoona huyu anafaidi yeye akajiita Yanga UMOJA WA MATAIFA na shabiki wao mmoja akawalipia wakatungiwa wimbo wa YANGA AFRICA UMOJA WA MATAIFA na Marehemu Peppe Kalle baada ya kuchukua ubingwa wa klabu bingwa Afrika mashariki pale Kampala Uganda Kwa kuifunga Sports Club Villa wakiwa chini ya udhamini wa Marehemu Abbas Gulamali Mbunge wa Kilombero.

Miaka 4 Hadi 6 iliyopita Simba walikuwa wanajitambulisha kama Simba MNYAMA wakatoa kofia, mizula, khanga na baadhi ya mashabiki wakawa na logo za MNYAMA. Ni kipindi hicho cha ufalme wa Simba chini ya ufadhili wa Mohamed Dewji "Mo" Pacha wake alipokuwa Hoi kiuchumi na kuendesha timu Kwa michango ya Wanachama wake alipoibuka na kauli mbiu ya "TIMU YA WANANCHI, MWEKEZAJI NI MWANANCHI". Mashabiki waliokuwa wanachangia timu wakaitwa "WANANCHI". Jambo hili likawa kubwa na likamvuta GSM kuwekeza baada ya kuona Fan base kubwa na hamasa ya kishabiki inavutia uwekezaji kwani angefanikiwa kutangaza na kuuza bidhaa zake kupitia nembo ya WANANCHI.

Kama ilivyo ada, Jana Pacha kajibadili naye kaamua kutumia slogan inayoendana na hiyo. Yeye anajiita MWENYE NCHI. Yaani kama wewe ni Mwananchi basi Mimi ni Mwenye nchi. Wanaojua kupima watapima na kuona faida na hasara za kudandia Slogan Tangu kipindi cha TAIFA KUBWA vs UMOJA WA MATAIFA Hadi Sasa MWANANCHI vs MWENYE NCHI.
 
Wenye nchi gani hao wakati hawakushiriki ktk hatakati za kupigania uhuru? Tena wengi waliokuwa na asili ya timu hiyo walikuwa upande wa wanyonyaji. Wamedandia jina lisilo na vinasaba nao
 
Simba ni wahaini!! Wanapojiita 'wenye nchi' ina maana hata mamlaka ziko chini yao🙄🙄? Maana hata rais wa nchi ni mwananchi sasa wao kama kikundi wanawezaje kumiliki nchi? Tafadhali watueleze nani aliewapa umiliki wa nchi yetu?

Halafu mkinga anaendelea na mikakati ya kumfukuza mhindi, kamfukuza kariakoo sasa anamfukuza kwenye klabu😂😂😂. Mo hajaamini kutokuona bidhaa yake hata 1 kwenye jezi mpya!!!
 
Wenye nchi gani hao wakati hawakushiriki ktk hatakati za kupigania uhuru? Tena wengi waliokuwa na asili ya timu hiyo walikuwa upande wa wanyonyaji. Wamedandia jina lisilo na vinasaba nao

Chief, yani mada inazungumzia simba na yanga na slogan zao kuanzia miaka wa 90's, wewe umeikokota mpaka kwenye mambo ya kupigania uhuru wa nchi miaka ya 60's!!!!??? Noma sana
 
Subiri watakueleza maana wana sababu ya kujiita WENYE NCHI.
 
Chief, yani mada inazungumzia simba na yanga na slogan zao kuanzia miaka wa 90's, wewe umeikokota mpaka kwenye mambo ya kupigania uhuru wa nchi miaka ya 60's!!!!??? Noma sana
Kweli ameenda mbali sana mkuu.
 
Wenye Nchi wanaweka Maslahi Ya Nchi mbele.

'Visit Tanzania'

Wananchi Wanaweka Maslahi Ya Klabu Mbele.

'Haier' = Visit Kidimbwi'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…