SoC02 Wenye nchi ni Wananchi: Dosari zilizo katika mifumo ya Kidemokrasia zinazoathiri dhana hii na utatuzi wake

Stories of Change - 2022 Competition

Gidius Kato

Member
Joined
Nov 5, 2021
Posts
6
Reaction score
4
UTANGULIZI
Ninayasoma maneno ya utangulizi yaliyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, maneno yaliyobainisha misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninagundua kwamba hata Katiba hii ya sasa ya mwaka 1977 licha ya mapungufu yake, inaendelea kuwataja WANANCHI kuwa ndiyo waamuzi katika ujenzi wa taifa lenye kuzingatia misingi haki, uhuru, udugu na amani na kwamba misingi hii itaweza kutekelezwa kwa kutumia DEMOKRASIA SHIRIKISHI (Representative Democracy) inayozingatia mfumo wa VYAMA VINGI kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Tanzania, 1977. Kwa kuzinatia mfumo huu wa demokrasia, je, wenye nchi ni wananchi?

DHANA YA “WENYE NCHI NI WANANCHI”
Taifa la Tanzania sio la viongozi wala watawala, wenye Tanzania ni watanzania. Watanzania ndio hupaswa kuamua kuhusu misingi sahihi ya upatikanaji wa viongozi wao, aina ya viongozi wanaowataka, mamlaka na madaraka ya viongozi hao, pamoja na ukomo wa madaraka ya viongozi hao. Viongozi hao wanapaswa kuwawakilisha wananchi na kufanya maamuzi KWA NIABA ya wananchi. kiongozi yoyote anayefanya maamuzi kwa niaba ya Wananchi haina maana kwamba maamuzi anayoyafanya ni ya mwisho na hayapaswi kupingwa, lazima iwepo mfumo wa kukataa maamuzi yanaonekana kukinzana na ustawi wa wananchi. Wananchi wanapaswa kuwa WANUFAIKA wa maamuzi hayo na sio kuwa WAHANGA.

Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetambua Dhana hii ya wenye nchi ni wananchi, katika ibara ya 8(1)(a)-(d). kwa kuwa Tanzania ni nchi iliyokubali kufuata misingi ya demokrasia, basi:
Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na mamlaka na madaraka yote ya serikali yatoke kwa wananchi.
Ustawi wa wananchi uwe ni lengo kuu la serikali.
Serikali inapaswa kuwajibika kwa wananchi
Kuwe na ushiriki wa wananchi katika shughuli za serikali yao.

Je, demokrasia shirikishi ya mfumo wa vyama vingi tuliyonayo nchini kwa maiaka 30 inalenga kuenenda na dhana hii? jibu, ni HAPANA. Bado zipo dosari katika mfumo wa demokrasia Tanzania, zinavyoathiri dhana ya wenye nchi ni wananchi.

DOSARI ZILIZO KATIKA MFUMO WA DEMOKRASIA NCHINI ZINAVYOATHIRI DHANA HII YA WENYE NCHI NI WANANCHI NA UTATUZI WAKE.
Taasisi zilizopewa mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa serikali zinajumuisha watendaji na wasimamizi ambao tayari ni wanufaika wa kuwa wananchama wa chama kimoja cha siasa. Mfano, Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni wanufaika wa uanachama wa chama tawala kuwa sehemu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Baadhi ya wagombea kutoka vyama vingine hususani ubunge, wamekuwa wakienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi huku ikihusishwa na sababu za kiitikadi. Wananchi hukosa fursa ya kumchagua kiongozi wanayemtaka wao na huamuliwa ni nani awe kiongozi wao kwa dhana ya KUPITA BILA KUPINGWA.

Ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki, nafasi za viongozi wa Tume na wasimamizi wa uchaguzi zitangazwe ziombwe na watu ambao hawana kazi yoyote serikalini au ndani ya chama cha siasa. Iwepo kamati maalumu ya kupitia maombi na kufanya usaili na kupitisha majina ya wanaostahili. Kamati hiyo ijumuishe majaji wenye uadilifu na wafanye kazi kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Mahakama.

Pia hata kama mgombea atabaki mmoja, Dhana ya kupita bila kupingwa tuizike na tuwe kiwango cha asilimia kadhaa cha kura za ndiyo. Iwapo atashindwa kufikisha asilimia hizo za kura, basi mchakato wa uchaguzi urudiwe tena katika eneo hilo la uchaguzi ili dhana ya WENYE NCHI NI WANANCHI iheshimiwe.

Zuio la kikatiba katika ibara ya 41(7) la kupinga matokeo ya Urais Mahakamani. Madhara ya zuio hili ni kwamba hata kama Rais aliyetangazwa hastahili kutangazwa, ama ushindi wake umepatikana kwa udanganyifu wa wazi basi mtu huyo ataapishwa kuwa Rais hata kama ni kinyume na maamuzi ya wananchi. Hivyo basi mamlaka na madaraka ya Rais huyo hayatoki kwa wananchi wenyewe.

Hivyo basi, Tanzania itekeleze maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu kuwa na utaratibu wa kuruhusu matokeo ya Urais kupingwa Mahakami iwapo kutakuwa na dosari katika uchaguzi wa kupatikana kwa Rais. Tunaweza kujifunza kwa wemzetu Kenya.

Wananchi wamewekewa mipaka ya namna ya kushiriki katika uchaguzi. Hii ni kwa sababu ya kuwataka wagombea wote wa nafasi za kuchaguliwa kuwa wananachama wa vyama vya siasa. Wapo wananchi ambao wanatamani kuwa viongozi na hawana kigezo hicho. Hii inamnyima mwenye nchi kupata fursa ya kuiongoza nchi yake na pia mwenye nchi anashurutishwa na mfumo kumchagua mtu anayetokana na chama cha siasa.

Pia Mbunge aliyechaguliwa na wananchi anaweza kuvuliwa ubunge kwa kuvuliwa uanachama na chama chake cha siasa. Mfano, iwapo ataikataa misimamo ya chama chake cha siasa ambayo haina tija kwa wananchi chama chake kinaweza kumvua uanachama kwa masuala ya kinidhamu. Hii inaathiri maamuzi ya wananchi ambao ni wenye nchi. Tunapaswa kuruhusu kuwa na Mgombea huru ili kutoa nafasi kwa wananchi ambao wanataka kuwa viongozi bila kupitia vyama vya siasa kuomba ridhaa kwa wananchi.

Maamuzi mengine yanayofanywa na Bunge kupitia aina hii ya Demokrasia Shirikishi hukinzana na ustawi wa wananchi. Wabunge wanapaswa kuishauri na kuisimamia serikali ili iwajibike kwa kuzingatia ustawi wa wananchi. Wawakilishi hupitisha miswada ya sheria, na kanuni hata kama ni kinyume na matakwa ya wananchi. Hakuna utaratibu wa wananchi kuwawajibisha wabunge wao ambao huenenda kinyume na ustawi wao mbali na kusubiri Uchaguzi Mkuu.

Mbaya zaidi baadhi ya maamuzi yakishafikiwa wananchi hawapewi msingi wa ufikiwaji wa uamuzi bali huona utekelezaji wa maamuzi. Wananchi wanapaswa kufahamishwa kuhusu sababu za kutaka kufanya maamuzi na maamuzi hayo yafanyike kwa kujali matakwa ya wananchi, iwapo wataenda kinyume iwepo mifumo ya kuwawezesha wananchi kuyakataa maamuzi hayo. Tuondoe utaratibu wa kufanya kila ya nyaraka zenye maamuzi kuwa za siri.

HITIMISHO.
bado kuna mapungufu katika mifumo ya kikatiba na hivyo katiba yenyewe imetambua dhana ya WENYE NCHI NI WANANCHI wa upande mmoja, na kuathiri dhana hiyo kwa upande mwingine. Tunahitaji kuwa na katiba mpya itakayotekeleza kwa ufanisi dhana hii hili wananchi wabaki na mamlaka yao.

Pia, tunahitaji kuwa na viongozi wanaoelewa sio tu Katiba (Constitution), bali pia maana ya Ukatiba (Constutionalism). Kuwa na katiba ni jambo moja, na ukatiba ni jambo linguine. Tunaweza kuwa na katiba nzuri sana yenye kutekeleza hii dhana lakini tukawa na viongozi wasiokuwa na hisia za ukatiba, wakashindwa kuelewa dhana hii.
 
Upvote 11

Mzigoooooooo[emoji109][emoji109]
 
Nawashukuru sana mliopiga kura. Mungu awabariki sana. Tuzidi kufanikisha hili andiko lipate ushawishi mkubwa katika shindano hili.

Utukufu una Mungu juu mbinguni
 
Back
Top Bottom