Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Watu wenye ulemavu kutoka mkoa wa Tabora wameeleza wasiwasi wao kuhusu mauaji yanayowakumba wenzao wenye ulemavu wa ngozi (Albino), wakisema kwamba baadhi ya watu bado wanashikilia imani potofu kuwa viungo vya Albino vinaweza kufanikisha mambo yao, hasa wakati wa chaguzi. Hofu hii imeongezeka kuelekea uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025.
Wakizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora, walemavu hao, Shaban Kaonbwe na Juma Maganga, wamesema mauaji haya yanatokana na imani zisizo na msingi ambazo zinawaweka walemavu wa ngozi katika hatari kubwa.
Sheikh Hussein Nkumilwa, ambaye pia amehutubia katika maadhimisho hayo, ameitaka jamii kuthamini maisha ya watu wenye ulemavu na kuacha mawazo ya kuwaondoa uhai kwa sababu za kishirikina.
Soma Pia: Barwan Salum: Walemavu watolewe hofu na wahamasishwe kuwania nafasi za uongozi
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Afisa Tarafa wa Tabora Kusini, Haika Masue, ameeleza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zinalindwa kwa nguvu zote.
Maadhimisho haya, ambayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 3 Desemba 2024, yanatoa wito kwa jamii kuwa na mtazamo chanya kuhusu walemavu na kuchukua hatua za kuondoa vitendo vya kikatili vinavyowakumba, hususan Albino.