Wenye uzoefu na haya mambo naomba mwongozo

TAI DUME

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
9,748
Reaction score
26,238
Habari ya Jumatatu
Ni hivi, miaka kama 6 iliyopitia nilitengeneza network moja ya kijasiriamali na watu wa nje ya bara la Africa. Nimeshafanya nao shughuli nyingi ambazo baadhi zilitulipa na nyingine zilikuwa na changamoto.

Sasa last year wameniambia niangalie uwezekano wa ku-invest ktk sekta ya mawasiliano hususani kuwekeza ktk makampuni ya simu kama halotel n.k. Capital ipo ya kuweza kuleta ushindani na hivo wamenitaka ikiwezekana niwe msimamizi wa uwekezaji huu kwa hapa Tz.

Mpk sasa nimefanya utafiti wa awali kwa maana ya taratibu za usajiri, ushindani soko ni, changamoto, tabia za walaji, gharama za kuanzia nk.

Changamoto ni kwamba sina uzoefu na sekta hii zaidi ya kuwa consumer. Hii nafasi niliyopendekezwa nahisi inanizidi umri maana kuwa msimamizi mkuu wa uwekezaji wa mabilion ya sh siyo kitu kidogo kwangu.

Wenye uzoefu na haya mambo hususani ktk sekta husika naomba mwongozo;
1. Ni aina gani ya watu Naweza kuwa contact hususani ktk kipindi hiki ambacho mradi upo ktk wazo kwa ajili ya kuboresha?
2. Ni aina gani ya watu Naweza kuwa contact kwa ajili ya kutengeneza business strategy?
3. Kwa upande wa technical issues, watu wa field ipi watafaa?

NB: These people are to be hired as soon as possible.

Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…