Wenye Zahanati binafsi mlioingia mkataba na NHIF huwa mnalipwa baada ya muda gani?

Wenye Zahanati binafsi mlioingia mkataba na NHIF huwa mnalipwa baada ya muda gani?

Hypersonic WMD

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
1,337
Reaction score
1,876
Wamiliki wa dispensary zinazopokea BIMA ZA NHIF huwa mnalipwa baada ya muda gani?


personal experience
Nilienda Aga khan Dar nikaona tangazo kua hawapokei NHIF labda zinazotoka bank kadhaa ila siyo NHIF ya kawaida.
Hivyo ilinijia akili kua hawa jamaa hawalipi kwa wakat na pia nishapata sana hayo malalamiko
 
Wamiliki wa dispensary zinazopokea BIMA ZA NHIF huwa mnalipwa baada ya muda gani?
Huwa kuna miongozo yao (mkataba ) ambao wametaja muda wa kulipwa baada ya kuwasilisha madai yako (claims). Sijui kama kila kituo (dispensary, health center au hospital) inakuwa na muda wake lakini nachojua ni kwamba kuna ambao malipo hulipwa baada ya siku 45 hadi 60 toka yanapowasilishwa kwenye ofisi zao.
 
Huwa kuna miongozo yao (mkataba ) ambao wametaja muda wa kulipwa baada ya kuwasilisha madai yako (claims). Sijui kama kila kituo (dispensary, health center au hospital) inakuwa na muda wake lakini nachojua ni kwamba kuna ambao malipo hulipwa baada ya siku 45 hadi 60 toka yanapowasilishwa kwenye ofisi zao.
siku 60 miezi miwili si unafirisika
 
Inaweza vuka hata miezi mitatu hivyo kuepuka kuyumba jitahidi uwe na mtaji mkubwa kidogo au mjitahidi kupeleka madai mapema tarehe 1 ,2 ..hapo itasaidia
Kama mdau hapo chini kasema wamelipwa mwaka jana wa 8 yaan mwaka mzima hujalipwa duuh
 
Mkuu,
Upo wap ? Kituo kipo dar es salaam. Wengi hu supply cheap brand za hapo India.

Biashara ya dawa za binadamu kwa wholesales inatajirisha Sana Ila mpaka uingie na uijue industry nje ndani ndio maana hata watu Kama Fred vunjabei kafanya diversity kutoka kwenye nguo.
Mfano
Let's say
Unanunua griseofulvin tabs 1box 10k unauza wholesale price 22k Aya tuseme griseofulvin ni SLOW MOVING ITEM.

Let's say
Fast moving items Ampiclox caps, amoxicillin caps, ciprofloxaciline tabs, doxycycline caps, pen v tab, paracetamol , metronidazole tabs dicloper tabs, azuma 500mg, erecto, rough rider condom, cefixime tabs, albendazole tabs, cephalexin tabs,toff plus caps, Alu alu 24 's, fluconazole caps/ tabs E.t.c

Hizi dawa zinatembea ni fast moving Sasa ukiweza kupata cheap brands ukaingia sokoni unatoboa kirahisi kabisaa.

Kuna fursa Sana upande huu watanzania wenzangu.
 
Mkuu kuhusu hii bima yetu ya NHIF ni majanga tu. Ukitegemea pesa ya Bima kuendeshea kituo utakifunga tu. Malipo kwa sasa wengine inawachukua hadi miezi sita. Na malipo yanakuja pungufu wakidai kwamba kuna udanganyifu na makosa yalifanyika katika utoaji wa tiba.


Kipindi cha nyuma Bima iliwafaidisha sana wenye vituo. Ila kwa sasa wengi wamevifunga baada ya mfuko kuyumba.

Na kituo bila bima utaishia kupima MRDT,URINALYSIS,UPT,WIDAL TEST,ESR na STOOL Analysis. Ni wachache sana wanaweza ku afford vipimo vikubwa kama FBP, SONOGRAPHY, RFT nk kwa cash.

Kwahiyo kama ni kituo kipya Keep hoping for the best but expecting the worst
 
Mimi nimepata muongozo wao ,nimesoma nikaishiwa nguvu, yaani PCM syrup wanalipa 1100,yaani Napata faida chini ya bati, aweee
Zipo.
Cheap brands Kama karamol@ 700syrup unaweza walau ambulia 450


Ila ukiweka sheladol, zenadol ,cetamol, cosmol,dolomol yaan hupati faida yeyote mfano kwa Sasa sheladol syrup @1720

Bei za nhif changamoto Sana..
 
Back
Top Bottom