Wenyeji wa Dar Es Salaam mtuchombeze kuhusu Dar

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Wenyeji wa Dar Es Salaam mtusaidie tuijue Dar.Mtuchombeze tujue Dar inakaaje.

Kwasababu huku country side tunasikiaga tu
Mara Buza kwa mpalange,mara Tandale kwa mtogole.

Mara matajiri wanaishi Masaki,
Mara Kariakoo ukiingia utaibiwa mpaka utalia..

Mara Sinza kwa ndo kwa wajanja
Mtusanue tuijue tusije kuonekana washamba siku tukija Dar...
 
si kila ukienda kariakoo utaibiwa, kwasababu wezi wenyewe wanaogopa kuiba kwwnye umati wa watu watauliwa, kariakoo ni salama na sehemu iliyochangamka na kufurahisha, achana na kununua nguo na vitu vyenginevyo, siku hizi kuna migahawa wanachakula kizuri mfano wali unaitwa mandi, kwahiyo kariakoo iko loa tu, masaki ndio wanakaa watu wenye maisha mazuri, ila sio hapo tu, mitaa mizuir iko kotekote jijini ikiwemo nauswahilini pia.

masaki ni sehemu nzuri kutwmbea, kuna miti yenye vivuli na ufuko wa coco beach, pamoja na club za elementz pamoja na samakisamaki, karibu dar, ni tanzania feel at home
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…