wenyeji wa Tanga mpo...?

Nenda Regal Naivera, au NYinda Annex, huduma bomba vyumba safi security juu parking swafi... ila usijaribu mkonge, hali si poa sana

a budget of 30-50k inakutosha kwa siku

...sawasawa mkuu,

Nyinda Annex ndipo hapo Next Level anapopasifia kwa kelele za Bar, Regal Naivera nayo naiweka kwa Diary, mnitaifanyia uchunguzi...

Dah, Mkonge Hotel inakandiwa namna hii? Imekuwaje jamani huko Tanga na wamiliki wake?!...
 

...naaam naaaam,

Inaonekana huyo muwekezaji (NYINDA) ana hoteli mbali mbali, mwanzoni nilimjudge kama nilivyoambiwa Bar mbele ya hoteli ni kelele tupu,...Kumbe kuna Annexe, Classic na Executive!!!

Nini recommendation yako, wapi panafaa ugeni mzito (watu wenye heshima zao)?...nisije kuaibika kupafagilia sehemu nisioijua!
 
 

Mbu, NYINDA ninayo ifahamu mimi ipo moja na ipo karibu sana na DOLPHIN Hotel....! pembeni ya hiyo Nyinda kuna bar huyo huyo jamaa (the same owner)! uzuri wa hii hotel ni tu rooms ziko nzuri sana, mpka kuna vi min bar kny vyumba vyao.....hapa ninapopafahamu kelele nyingi sana mkuu!

BWT: Kama wageni wako ni WAZUNGUs fulani .....wapeleke tu Mkonge, vitu tunavyomind si wengine vinaweza kuwa si issue kubwa kwao, na ofcoz pale nikuta na wenzao kibao...pengine wao wanahudumiwa vizuri zaidi...si unajua si waswahili....?
 


Exactly mkuu NL, mkonge nilikuwepo mwaka 2006 sasa walipoitaja hapa nikasita kuikandia nikidhani huenda wamebadilika, lakini wapi...bado kumbe wana ile mentality ya mashirika ya Umma..so hawapo kibiashara hata kama 'imebinafsihwa'.

Dolphin kweli parking ndogo lakini ni nadra ukose parking pale unless una lori, lakini nadhani parking ipo, kuhusu vyumba ni sawa kabisa ulivosema,,

hizo nyinda zipo nyingi na the same area lakini pia kuna nyingine zipo maeneo hayo hayo so ukikosa sehemu moja ni rahisi kucheki nyingine hata kwa miguu.

Mkuu NL yale mambo mengine vipi ukiacha malazi? ukarimu wa wenyeji (au mkuu Mbu amefunga)
 

NL, kuna nyinda nyingine mpya [executive] ni nzuri... ila muwe makini sana na Tanga, wanawake wa Tanga ni wezi kuliko sehemu yoyote Tz; majamaa ya workshop mengi yanakoma aisee
 
 
Ipo hotel nyingine INN BY THE SEA, ni nzuri tu ipo baharini,waweza jaribu pia na hiyo mbu!
 

Kakosea spelling huyo. Hakuna Panora hotel Tanga inaitwa PANORI. I have been there thrice, pametulia sana. Pia hapo kiboko hotel pametulia na feature special niliyoona ni ile mishkaki yao jinsi wanavyoichoma kwa umahiri. Nshakula, nshalala pale pia.
 


Thanks Mkuu, hiyo Nyinda unayoisema its more of a guest house na pembeni wana sehemu ya tropper nzuri sana... lakini ile nyingine ni bomba zaidi
 

Kweli wewe unazo habari za motomoto. Hivi Chichi siku hizi kumekua kizuri nako? Nina siku nyingi nipo humu magomeni sijafika huko aisee. Umenitamanisha sana samaki aina ya changu pale ulipotaja deep sea. Kesho naja huko kwa raha leo mkuu. Tukutane nyinda,agiza mguu wa mbuzi na ndizi.
 
...Mkuu NL yale mambo mengine vipi ukiacha malazi? ukarimu wa wenyeji (au mkuu Mbu amefunga)

...ha ha ha, naaam swaumu imepanda hapa kama kwao,...bado masaa mawili na ushee hapa nile mahanjumati!...

NL, kuna nyinda nyingine mpya [executive] ni nzuri... ila muwe makini sana na Tanga, wanawake wa Tanga ni wezi kuliko sehemu yoyote Tz; majamaa ya workshop mengi yanakoma aisee

...ebanaa weeeh, kumbe ni kweli Tanga nyumbani kwa mijizi? nimeifuma hii sasa hivi mahala fulani mama wa kizungu analalama
...inabidi kwenda na risasi za ziada huko...! πŸ™‚

Ipo hotel nyingine INN BY THE SEA, ni nzuri tu ipo baharini,waweza jaribu pia na hiyo mbu!

...Omumura, ubarikiwe sana. So far so good, responce za wadau zinatia matumaini kwamba kumbe kuna chaguo la kutosha zaidi ya Mkonge Hotel kwenye wahudumu wachafu!...

Next Level, ushauri wako nauzingatia kwa makini, umenifumbua macho sana kuhusu mji huo,...

Kaizer, huu mwezi wa toba yakhe! sijui hata kama Mw'mungu amenisamehe wewe unataka nianze kufikiria kujiexpress upya, ha ha haa....
 


mkuu ungemalizia kabisa swali letu kwa kuwaulizia ""jolly club ""ya tanga ipo wapi kwani hata mimi nategemea kufika huko mwezi ujao...ni juzeni wakuu..!!
 
mkuu ungemalizia kabisa swali letu kwa kuwaulizia ""jolly club ""ya tanga ipo wapi kwani hata mimi nategemea kufika huko mwezi ujao...ni juzeni wakuu..!!

...ha ha ha...

Next Level amesema; "Mbu kama mwenyewe unaenda Tanga na hupenda kujirusha, pitia pale Club la Casa (ni night club), is very nice place kwa wanaopenda kujirusha mkuu!"

....,au kwa taarifa zaidi muume sikio (mtumie PM) Kaizer, yeye mbado kuuona mwezi! πŸ™‚
 
mkuu ungemalizia kabisa swali letu kwa kuwaulizia ""jolly club ""ya tanga ipo wapi kwani hata mimi nategemea kufika huko mwezi ujao...ni juzeni wakuu..!!

Ni opposite na posta pale. Au wenyewe wanapaita Independence Avenue. Unapanda pale ghorofa ya kwanza tu mzee. Kwanza mida ikishafika wewe nenda pale posta macho yatafuatilia yenyewe automatically maana utaona pilika za watu kuelekea club hapo. Au nenda zako coffee bar katulie. Ikifika tano na nusu hivi nenda moja kwa moja, pale four ways vuka fuata bara bara moja kwa moja kuelekea posta. Tena kuna members wengi sana hua wanaongozana kutoka coffee. Na mambo fulani ni jirani kabisa pale,mitaa ya Makundi.
 

Ha!ha!ha!ha!ha!....mkuu Bao3......Pale Chichi pamepoza kidogo...halafu watch out ......kuna wale waheshimiwa wa ''MOMBASA'' acha kabisa unaweza uziwa mbuzi kny gunia usijue kabisa.....!

Deep Sea achana nako kabisa, ukitaka shuka kabisa baharini huko utakutana na the likes of Tasi, changu, kibuas etc....raha tupu kule!

mkuu ungemalizia kabisa swali letu kwa kuwaulizia ""jolly club ""ya tanga ipo wapi kwani hata mimi nategemea kufika huko mwezi ujao...ni juzeni wakuu..!!

Mkuu, Club La Casa....Chichi...mwisho wa yote ..ha!ha!ha!


Naaaaaaam....yakhee naona umenipata vilivyo......but watch out Tanga kuna ''BWABWA'' sana....usinunue mbuzi kwenye gunia...ha!ha!ha!
 

...ha ha ha...kama mbuzi vile wakielekea machinjioni! duuuh,

itabidi nikachungulie hiyo mitaa ya posta, lakini nitahakikisha najifunga na kamba kwenye nguzo ya stima nisiwafuate!
 
...mmmm, kweli Tanga nimetoka muda mrefu! whatever happened to my favorite staying place in the early 90 'Inn by the Sea' mitaa ya huko huko Mkonge Hotel, ama ipo ila ndio mambo ya kubadilisha jezi mchezaji yule yule?? Na Tanga Hotel je? Na zile hoteli za yule mjasiriamali aliyepata kuwika sana pale Tanga, Marupa, moja ilikuwa pale keepleft cha Chumbageni Police??
 

Ha!Ha!Ha!ha!ha!ha!....hapo Tanga hotel.....ni maarufu kwa vikao vya harusi, send off, ''chicken'' party etc! ....na ofcourse weekend kuna live band pale ndani......but si pazuri kwa kulala ati!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…