SoC03 Wenyeviti vitongoji walipwe kuboresha uwajibikaji

SoC03 Wenyeviti vitongoji walipwe kuboresha uwajibikaji

Stories of Change - 2023 Competition

achaniseme2

New Member
Joined
Jul 27, 2023
Posts
2
Reaction score
2
SERIKALI za Mitaa hutafsiriwa kama vyombo vya wananchi ambavyo huundwa kwa ajili ya kuwajibika kwa wananchi.

Hapa nchini vyombo hivi vimeanzishwa kwa Ibara ya 145 na 146 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, Sura ya 2 zinazobeba dhana ya ugatuzi wa madaraka ikiwa ni sehemu ya serikali iliyokaribu na Wananchi.

CHANGAMOTO
Pamoja na kuundwa kwa lengo jema la kuwajibika kwa Wananchi ila sehemu kubwa ya wenyeviti wa vitongoji/serikali za mitaa wamekuwa sababu ya maumivu kwa Wananchi.
Kwani imekuwa ni jambo la kawaida kuwasikia mawaziri wenye dhamana ya ardhi, wakikemea Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kujihusha na uuzaji wa viwanja na mashamba katika maeneo wanayoongoza.

Wenyeviti wengi wa vitongoji wamekuwa chanzo cha migogoro kwani wengine wamekuwa hadi mashahidi wa wanunuzi wa ardhi za mgogoro huku wakijua kufanya hivyo huchochea ongezeko la migogoro.

Changamoto nyingine ambayo imekuwa sugu kwa Wananchi kutoka kwa Wenyeviti hawa ni suala la kudai asilimia 10 ya mauzo ya viwanja huku wakijua suala hilo ni kosa kisheria.

Ofisi za wenyeviti hawa zimegeuka kuwa sehemu ya huduma kwa wenye fedha kutokana na kila huduma kutolewa kwa kulipia kama vile; barua ya utambulisho wa wakazi wanaotaka huduma za kuunganishiwa maji, umeme, dhamana polisi, kuomba kazi au mikopo.

Tatizo jingine ni kutokuwepo kwa kiwango cha elimu stahiki kwa viongozi hao, kwani hilo limechangia kuwa na viongozi ambao wamekuwa wakifanya makosa kutokana na uwezo wao mdogo wa kupambanua mambo hasa ya kimaendeleo katika eneo husika.

Changamoto nyingine wanayokutana nayo ni kukosekana kwa vyanzo vya mapato kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi, hali inayowafanya kujikuta wakitumbukia kwenye vitendo vya rushwa.

Pia hata halmashauri kutopeleka rasilimali watu, fedha na vitendeakazi.

NINI KIFANYIKE
Jambo kubwa serikali inatakiwa kutengeneza utaratibu wa kuwalipa posho au mishahara wenyeviti hawa ikiwemo na kuwapa fungu la kununua vitendeakazi.

Iwapo serikali itafanya hivyo itasaidia viongozi hao kuachana na tabia ya kuomba rushwa kwa Wananchi hali inayosababisha kuwanyima haki ya kuwahudumia wale wasiokuwa na rushwa.

Pili kutoa semina elekezi kwa Wenyeviti wa vitongoji kutambua majukumu yao ya kiutendaji katika majukumu yao kwa jamii wanayoiongoza.

Serikali itazame upya sifa za kutangaza kiwango cha elimu kwa wagombea wa nafasi hizi ili kupunguza kuwa na viongozi wenye uwezo mdogo wa kufikiri kiasi cha kuchangia kuuza hata maeneo ya maendeleo kwa lengo la kujinufaisha binafsi.

Picha
Sehemu ya shamba katika eneo la Razaba Bagamoyo ambalo linadaiwa kuwa Mali ya Serikali ya Zanzibar lakini kwa sasa wananchi wanalitumia Kwa kilimo na makazi
IMG_20230211_181233_635.jpg
 
Upvote 0
Back
Top Bottom