Pre GE2025 Wenyeviti wa Mitaa Jimbo la Temeke waungana kumuombea dua Rais Samia kwa lengo la kumtakia afya njema

Pre GE2025 Wenyeviti wa Mitaa Jimbo la Temeke waungana kumuombea dua Rais Samia kwa lengo la kumtakia afya njema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Wenyeviti wa mitaa wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, wameungana kwa pamoja kumuombea dua Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kumtakia afya njema, hekima na uongozi mwema ili aendelee kuiongoza nchi kwa amani na kuleta maendeleo.

Soma pia: Picha: Viongozi wa Dini wakiwa viwanja vya Leaders, Kuliombea Taifa Amani na Rais Samia Suluhu Hassan


Nimeacha kutazama aliposema nchi yetu amani ilivyo. Quran, Biblia na vitabu vingine vipo ila watanzania wanamuabudu shetani huku wakijivika hizi imani. Hawa ndiyo akina FaizaFixy FaizaFoxy .Awamu ya 5 walipouwawa watu si sawa, ila awamu ya sita wakipotezwa na kuuliwa aaah, amani tele
 
Bora wangefanya dua ya kudai Katiba mpya
 
Kwani yeye mwenyewe hawezi kujiombea hadi aombewe, huu uchawa umezidi sasa jamani hebu oneni aibu.
 
Huko Temeke maji yanatoka? Viongozi mnapata nafasi ya kumfikishia ujumbe Rais mnafanya Uchawa?
 
Yule mwingine aliombewa na akaomba cheo cha kuongoza malaika na yakawa.
 
Kuna mda haya maombi mnafanya ofisi ya mtoa roho huko mbinguni kuwa inapokea request nyingi kujua huyu ni nani huko
 
Back
Top Bottom