Wenyeviti wa Serikali za mitaa, vijiji, vitongoji muda wenu umekwisha, Je adui yenu ni CCM au Serikali?

chuuma

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2015
Posts
363
Reaction score
557
Na Boniface Jacob
Senior councillor

Jana tarehe 22 October 2019 Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji pamoja na Wajumbe wao Wamemaliza Muda wao wa Miaka 5 Tangu wachaguliwe Mwaka 2014 Muda kama huu kwa Mujibu wa Sheria namba 8 na 9 za mwaka 1982 (Sura 288)

Kiutendaji jana ndiyo ilikuwa siku ya Viongozi hao Kurudisha Mihuri ambayo ndiyo inasadifu Mamlaka na Madaraka yao katika Utendaji wao wa Kazi za Kila siku.

Mihuri hiyo hutumika kuidhinishia na kutia rakiri katika Nyaraka mbali mbali za wafuata huduma au Nyaraka za Serikali.

Jana ndiyo Mwisho wao pia wa kutoa Maelekezo au amri kwa mtendaji wa Kijiji au Mtaa katika eneo alilokuwa amechaguliwa na wananchi wakazi husika kuwaongoza katika mambo mbali mbali.

Kwa Bahati mbaya wengi awajui kuwa Siyo tuh wenyeviti wa Mitaa,Vijiji na Vitongoji bali zoezi la kukoma kwa Muda,mamlaka na Madaraka linawahusu pia wajumbe wa Serikali za Mitaa na vijiji ambao kwa Pamoja ndiyo wanaunda chombo kinaitwa "Serikali ya Mtaa" au "Serikali ya Kijiji"

Leo nataka kutumia kalamu yangu kuwa Fikishia Ujumbe wa Machungu kutoka kwenye Vifua vya wastaafu hawa wa Serikali za Mitaa

Je kukoma kwao kwa Uongozi ndiyo kukoma kwao kwa thamani yao katika kipindi chao cha Miaka 5 waliyo watumikia Wananchi na Nchi yao?

Serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji zimekuwa na Mchango Mkubwa Sana katika kuchochea Maendeleo ya wananchi Nchini kote.

Majukumu kama ulinzi na Usalama,Uangalizi wa miundombinu,usimamizi wa Ardhi,Usimamiaji wa Usafi,Uangalizi wa Ustawi wa Jamii,Utambuzi wa Jinai na dhamana za watu wao,pamoja na usimamiaji na utekelezaki wa Maagizo ya Serikali.

Lakini Thamani ya Kundi hili adimu na la upekee limeshindwa kuonekana siyo tuh kwa Chama Tawala kinachojinadi kusimamia Ilani yao ya Uchaguzi,

Bali Hata serikali Kuu ambayo ndiyo wanaonufaika na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji Kwa Nchi Nzima.

Wenzetu wanaondoka baada ya Utumishi wa Miaka 5 ya lawama,fedheha na Manyanyaso kutoka kwa Viongozi wa serikali kama Wakuu wa Mikoa na wakuu wa wilaya,ambao huwatumia hawa viongozi kama "punching bag" katika kujifunzia kazi uwaweka mahabusu na muda Mwingine kuwadhalilisha hadharani mbele ya waliowachagua.

Lakini kubwa Zaidi hakuna kiongozi yoyote wa Chama tawala ameshajitokeza hadharani hadi sasa kuongele Maslahi ya Wenyeviti wa Serikali za mitaa,Vijiji na Vitongoji pamoja na Kazi nzito waliyofanya kwa Miaka 5.

Pamoja na kuwa Viongozi wa Chama na Serikali wanajua fika maslahi duni ya watu hawa wanaofanya kazi usiku na Mchana kuhakikisha Nchi yetu inakuwa Salama

Lakini wamekuwa hawalipwi Mishahara na kwamba kazi yao ni yakujitolea,Miongozo inaonyesha kuwa walipwe Posho ya 50 elfu kwa Mwezi kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji huku wale wajumbe wanaounda Serikali katika maeneo hayo wanalipwa shillingi Elfu tano tuh kila Mwezi.

Mbaya zaidi wenyeviti wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji hawana kiinua Mgongo kama wabunge wanao ondoka na zaidi ya Millioni 200 huku Madiwani wakiondoka na zaidi ya Millioni 10 kila wanapomaliza utumishi wao wa miaka 5.

Wenyeviti hawa ndiyo ambao wamekuwa Nguzo kubwa na Msaada sana katika chama tawala na Serikali kuu hasa katika Vipindi vya Uchaguzi Mkuu, ambapo wao pekee wanakuwa tayari Madarakani au wakati wa Kuendesha Mazoezi ya serikali kama vile sensa , Kumbe wenzao huwachukulia kama Makarai ya kutafutia Madaraka tuh

Wamesahaulika hawana thamani sawa na wanasiasa wengine katika Nchi hiyohiyo Moja.

Waziri wa TAMISEMI Bw Suleiman Jaffo amejitokeza Kuongelea Ukomo wa Siku ya Mwisho kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji lakini haongelei kuhusu kishika Mkono,Asante wala kiinua Mgongo kwa Watu hawa wanaojua Shida zetu na waliokaribu na wananchi kuliko hao wanasiasa wanaogharamiwa ma Millioni ya pesa wakati hawaonekani hata Mitaani kwa wananchi.

Ukiondoa Utaratibu binafsi uliowekwa kwa Halmashauri za Dsm pekee kama Ubungo ma Kinondoni wa kuwatengea kiasi kidogo cha Asante,

Hakuna mkoa Mwingine wala halmashuri yoyote yenye utaratibu kama huu kwa kile kinachosemekana wanaogopa,awajui Msimamo wa Mwenyekiti wa CCM na Mheshimiwa Rais katika Jambo hili.

Serikali ilipaswa kutoa Mwongozo kwa Halmashauri zote nchini kuweka utaratibu wa Kishika Mkono au Mkono na Asante kwa Wale wenyeviti wa Serikali za mitaa Vijiji na Vitongoji

Hii ingesaidia hata hao wapya wanaokuja kuwa na hali ya uwajibikaji katika utendaji kazi na uadilifu kazini baada ya kuchaguliwa kuwa Viongozi tena hapo November 24.

Lakini Ukimya wa Rais Magufuli Mwenye dhamana na TAMISENI na Waziri wake Suleiman Jaffo katika jambo hili bila shala limefanya Wenyeviti wajue kuwa Wenzao na Mabosi wao hao huwatumia kama Karai wakati wa kutafuta Madaraka,na baada ya kupata Madaraka husaulika kabisa

na Sasa watakuwa wanamjua adui wao ni nani kati ya CCM na Serikali.
IMG-20191023-WA0039.jpg
 
Kuna baadhi ya wakuu wa wilaya wanawaona viongozi hawa wa vijiji, mitaa na vitongoji kama watumishi wao wa ndani!
 
na Sasa watakuwa wanamjua adui wao ni nani kati ya CCM na Serikali.View attachment 1241646
Ni ukweli unao umiza lakini tambueni Serikali chini ya CCM ni ya ubinafsi hata chembe ya huruma haina
Wanajinadi ni serikali ya wanyonge sijui wanyonge wapi ?
Au ukitembea na v8 au v10 ndio unyonge?
 
Ndugu umeongea kwa hisia na ukweli mtupu. Mie takupa mfano hai mmoja kutoka kwa mwenyekiti mmoja anayetoka katika halmshauri ya wilaya ya Msalala Shinyanga. Hadi jana wanaambiwa kurudisha mihuri walikuwa hawajaambiwa kama endapo watalipwa posho zao za miaka mitano madarakani huku halmashauri hiyo ikitajwa moja ya halmashauri zilizofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato awamu hii.
Nilichojifunza Serikali hasa ya CCM ni Serikali isiyojali watu wake wa chini isipokuwa kuwatumikisha tu. Nashangaa imetumia nguvu nyingi kuhamasisha watu wakapige kura huku ikifahamu watu wanaoenda kuchaguliwa ni sawa na kalai la kubebea tope la simenti wakati wa ujenzi
 
Nilikua nimejipanga kugombea ila kwa nondo hizi naondoa jina langu bora nikawe chinga mtaani kuliko huu utumwa mambo leo ambao taifa limeshindwa kutambua kazi ngumu ya wenyeviti wa mtaa na vijiji ata kuwapa kifuta jasho cha milioni moja tu
 
Hii nondo imesimama kwelikweli! Nilikuwa sijui kama mwongozo unaonesha kabisa malipo ya hawa viongozi.

Siku watanzania wote tukipata elimu hii mabadiliko tutayafanya wenyewe bila hata kusubiri wapinzani wapigwe risasi, watekwe/wapotezwe, wabambikiziwe kesi au kunyanyaswa kwa namna yoyote ile wakitutetea sisi
 
Back
Top Bottom