Mbunge wa Jimbo la Msalala mkoani Shinyanga, Iddi Kasimu amewapatia usafiri wa baiskeli bure wenyeviti wa serikali za vijiji 92 vya halmashauri ya Msalala, utakaowasaidia kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao zenye thamani ya TSh. Milioni 23.
Baiskeli hizo zimekabidhiwa leo Mei 4, 2025 na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Kawaida, baada ya kuwahutubia wananchi wa kata ya Bugarama halmashauri ya Msalala na kuwaeleza namna serikali inavyotekeleza miradi inayogusa maisha ya wananchi huku akiwasisitiza kuilinda na kuitunza ili iwanufaishe.
Amempongeza mbunge kwa kuona umuhimu wa kuwapatia usafiri wenyeviti wote wa serikali za mitaa kwa lengo moja la kufautilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwataka wengine kuiga mfano huo ili kuwa pamoja na viongozi wao ambao kwa asilimia kubwa wako karibu na wananchi.
"Ninakupongeza sana kwa hatua hii ya kuwafikia wenyeviti wa serikali za mitaa na kuwapatia usafiri, tangu nimeanza ziara yangu ya siku 10 sijakutana na tukio la namna hii; Wenyeviti tumieni baiskeli hizo kwa malengo yaliyokusudiwa" ameongeza Ali.
Hizi ni dharau sasa , Hiyo.Miradi si ya Serikali wabunge wakiwa wanafuatilia miradi ya serikali wanakwendaje.
Hako kajamaa kaseme tu kameamua kuwapa rushwa wakachague tena