Don Gorgon
Member
- Nov 21, 2024
- 35
- 68
Wenyeviti wa Mitaa wateule 106 kutoka katika kata 20 za Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wanaapishwa leo Novemba 28, 2024 katika Ukumbi wa Soko Kuu la Magomeni.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Kinondoni ambaye pia ni Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Hanifa Hamza ndiye mgeni rasmi katika tukio la kuapishwa kwa wenyeviti hao 106 pamoja na wajumbe 530.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na manispaa hiyo, wenyeviti wa mitaa wateule 106 wanaotarajiwa kuapishwa katika tukio hilo wote ni kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pia, soma: LIVE - LGE2024 - Special Thread: Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024