Binafsi sisemi wasipewe lakini naiangalia tu hii Dunia yetu najiuliza mambo mengi sana. MAMBO MAKUBWA YENYE KUSHANGAZA NA KUSTAAJABISHA.
Ila ninawaza ni kwanini mke wa DAKTARI asilipwe mafao kutokana na ugumu wa kazi ya mume wake. Mwanamke wa DAKTARI ana kazi kubwa sana ya kumuhudumia mwenza wake kimwili na kisaikolojia maana mtu anarudi nyumbani hana mood kabisa kutokana na kumuhudumia mgonjwa mwenye changamoto za ajabu
MAMBO YANAYOENDELEA KWA BAADHI YA NCHI HAPA DUNIANI HUWA NAWAZA NA KUTAMANI NI HERI MWENYEZI MUNGU AIFANYIE MAREKEBISHO HII DUNIA ILI DUNIA IPATE WATU WATAKAOGUSWA NA MAISHA YA WENZAO NA SIO WAO TU. ALETE WATAWALA WA AINA YA NYERERE AMBAO HAWATAJIANGALIA WAO BALI WATAKAOWAANGALIA WANANCHI WAO.
NI KWELI Mwananchi wa kawaida au mtumishi huwezi kuwa na privilege sawa na Rais, Waziri, Mbunge nk, lakini huwa nikiangalia maslahi ya viongozi wetu halafu bado familia inapigania nayo ilipwe daaah!!!!! Nikiangalia mafao ya wabunge wetu baada ya miaka mitano nikilinganisha na wanachokifanya bungeni daaah!!!! Kwanza sijawahi kuona wabunge wakisimama kwa nguvu moja kuwatetea watumishi wa uma kuboreshewa maslahi.
MUNGU WA MBINGUNI IANGALIE NCHI YAKO YA TANZANIA . IPATIE VIONGOZI WAKILA NYAMA BASI NAO WATATAMANI WANANCHI WA NAO WALE NYAMA