Wenzangu mnaridhishwa na ujenzi wa barabara ya mwendokasi njia ya Posta-Mwenge-Ubungo-Tegeta?

Wenzangu mnaridhishwa na ujenzi wa barabara ya mwendokasi njia ya Posta-Mwenge-Ubungo-Tegeta?

Pendragon24

Member
Joined
Aug 8, 2018
Posts
68
Reaction score
97
Mimi binafsi sioni kabisa kinachofanyika katika ujenzi wa barabara ya mwendo kasi kwa phase hii ya njia ya tegeta posta na kipande cha ubungo tofauti kabisa na ujenzi wa njia ya Morogoro road au ilee ya gongolamboto.

Enzi za ujenzi wa Morogoro road kwanza utaona watu wapo busy masaa 24 kufanya kazi hata vifaa vya kazi vilikuwa vimejaa ndani ya sati wafanyakazi wana full PPE sio huu wa tegeta.

Mradi huu wa tegeta kila siku wao ni kuchimbua chimbua tu na kutuzalishia mafoleni yasiokuwa na tija yaani ni kama mkandarasi halipwi kazi ya ovyo vifaa tu anavyotumia na mitambo imechoka sijui anakodisha kwa bei nafuu yaani ni upuuzi mtupu.

Unaeza kupita ukakuta wafanyakazi wanachota maji kwenye mandoo wana mwaga barabardani mpaka unajiuliza huu mradi vipi mbona ujanja ujanja wa wazi.

Kiukweli Huu ujenzi unadanadana nyingi sana na umekaa kichovu chovu sana. wahusika wawe serious kama kweli wamekusudia kuukamilisha.
 
Back
Top Bottom