Wenzetu wanafanikiwa kwa sababu wanawaza "endapo kitatokea"sisi tunafeli kwa kuwaza "hakitatokea"

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Waswahili ama waafrika tuna ujinga wa kuwaza "hakuna kitakachotokea" ndio maana mambo mengi tunafeli.

Wakati wenzetu walioendelea wanawaza kwamba "kitatokea kitu".

Mswahili haoni shida kuendesha gari hajafunga mkanda hawazi kabisa kwamba endapo ikitokea ajali bila kufunga mkanda naweza nikarushwa kutoka kwenye siti yangu mpaka nje na nikafa,yeye hawazi.

Wenzetu wakiingia kwemye gari wako makini kufunga mikanda kwa sababu wanawaza kwamba endapo itatokea ajali hapa huu mkanda utanisaidia kwa namna kadhaa wa kadhaa.

Mswahili anaamini kwamba kuwaza endapo kitatokea kitu kibaya basi kuwaza huko ni uchuro kabisa hivyo tachukui tahadhari juu ya hatari ambayo pengine inaweza kutokea.

Mswahili sio ajabu akakwea pikipiki bila kuvaa helmenti akiamini hakuna kitakachotokea huku akijifariji kwamba kuwaza kutokea jaali ni ichuro hivyo hachukui tahadhari,matokeo yake aji ya kawaida ikitokea anapasuka kichwa naaondoka.....

Wenzetu helmeti wanalipa kipaumbele kwa kuamini sana kwamba lolote linaweza kutokea.

Sehemu ya biashara kubwa za watu wanafanya kisha hakuna chanzo chochote cha maji cha uhakika kujilinda na majanga ya moto huku ni kuwaza kwamba hakuna kitakachotokea tuko safe.

Matokeo yake matatizo ya moto yakitokea inakuwa ngumu kucontrol moto usisambae na lawama atarushiwa kila mtu wakati kimsingi kuna mtu ndio chanzo kikuu.

Kuna tajiri alijenga ghorofa kama sikosei,madirisha kayapiga ulinzi mkali wa nondo na full security kiasi kwqmba mwizi hapiti,siku nyumbaa iungua moto watu hawajui wapite wapi kumuokoa jamaa aliungua na familia yake kama maskhara.

Watu hawafikirii kabisa kwamba sawa unaepusha jambo fulani lakini kuna jambo lingine endapo litatokea.

Unapoweka ulinzi dhidi ya maadui wa nnje wasiingie ndani,je unahakikishaje kwamba wewe wakitokea maadui wa ndani utaweza kutoka nje haraka na kujiokoa ?

Mswahili anaamini kwamba maisha yako safe sana,nothing will happen na anything kikihappen anahaha sana kutafuta msaada lakini it's too late.

Mwisho naomba kila mmoja ahakikishe kwamba pale alipo anakuwa ameweka tahadhar dhidi ya majanga ya kawaida endapo yatatokea basi aweze kuyadhibiti na kuepusha madhara zaidi.
 
Upo sahihi kaka mkubwa pia kwenye suala la bima ya afya watu hawakati bima at least ya watoto wao ile ya 50400/- wakiamin hawataumwa matokeo mtoto akiumwa uchumi wa familia unayumba kabisa au mtoto kushindwa kutibiwa
 
Hiyo ndo inaitwa kuwaza hakuna kitakachotokea.

Wabongo wengi huwa tunawaza hivi hata kama uhalisia uko kinyume na sisi.

Ndio maana hata saving tu kwetu inakuwa shida
 
Waswahili ama waafrika tuna ujinga wa kuwaza "hakuna kitakachotokea" ndio maana mambo mengi tunafeli.

Wakati wenzetu walioendelea wanawaza kwamba "kitatokea kitu".

Mswahili haoni shida kuendesha gari hajafunga mkanda hawazi kabisa kwamba endapo ikitokea ajali bila kufunga mkanda naweza nikarushwa kutoka kwenye siti yangu mpaka nje na nikafa,yeye hawazi.

Wenzetu wakiingia kwemye gari wako makini kufunga mikanda kwa sababu wanawaza kwamba endapo itatokea ajali hapa huu mkanda utanisaidia kwa namna kadhaa wa kadhaa.

Mswahili anaamini kwamba kuwaza endapo kitatokea kitu kibaya basi kuwaza huko ni uchuro kabisa hivyo tachukui tahadhari juu ya hatari ambayo pengine inaweza kutokea.

Mswahili sio ajabu akakwea pikipiki bila kuvaa helmenti akiamini hakuna kitakachotokea huku akijifariji kwamba kuwaza kutokea jaali ni ichuro hivyo hachukui tahadhari,matokeo yake aji ya kawaida ikitokea anapasuka kichwa naaondoka.....

Wenzetu helmeti wanalipa kipaumbele kwa kuamini sana kwamba lolote linaweza kutokea.

Sehemu ya biashara kubwa za watu wanafanya kisha hakuna chanzo chochote cha maji cha uhakika kujilinda na majanga ya moto huku ni kuwaza kwamba hakuna kitakachotokea tuko safe.

Matokeo yake matatizo ya moto yakitokea inakuwa ngumu kucontrol moto usisambae na lawama atarushiwa kila mtu wakati kimsingi kuna mtu ndio chanzo kikuu.

Kuna tajiri alijenga ghorofa kama sikosei,madirisha kayapiga ulinzi mkali wa nondo na full security kiasi kwqmba mwizi hapiti,siku nyumbaa iungua moto watu hawajui wapite wapi kumuokoa jamaa aliungua na familia yake kama maskhara.

Watu hawafikirii kabisa kwamba sawa unaepusha jambo fulani lakini kuna jambo lingine endapo litatokea.

Unapoweka ulinzi dhidi ya maadui wa nnje wasiingie ndani,je unahakikishaje kwamba wewe wakitokea maadui wa ndani utaweza kutoka nje haraka na kujiokoa ?

Mswahili anaamini kwamba maisha yako safe sana,nothing will happen na anything kikihappen anahaha sana kutafuta msaada lakini it's too late.

Mwisho naomba kila mmoja ahakikishe kwamba pale alipo anakuwa ameweka tahadhar dhidi ya majanga ya kawaida endapo yatatokea basi aweze kuyadhibiti na kuepusha madhara zaidi.
Katika mukhtadha huo huo, wenzetu huweka akiba, iwe ni pesa au mali, na ardhi, wakitegemea hapo baadae, fursa au mahitaji yatakuwepo au kutokea. Kwa upande wetu, tunaponda mali, fedha tukiamini kifo chaja, tutawafaidisha wengine. Matokeo yake hata ujenzi, mfano wa barabara, hatuachi nafasi kwa ajili ya upanuzi ili hapo baadae nikiwa na mahitaji zaidi, barabara ipanuliwe, tunaifinya, na baadae, tunawabomolea waliowekeza pembezoni, na kulipa fidia, gharama inakuwa kubwa maradufu.
 
Hiyo ndo inaitwa kuwaza hakuna kitakachotokea.

Wabongo wengi huwa tunawaza hivi hata kama uhalisia uko kinyume na sisi.

Ndio maana hata saving tu kwetu inakuwa shida
Ya mlo 1 tu shida, ya saving itatoka wapi?
 
Back
Top Bottom