Ukiachana na sababu za kidini kufunga kiujumla sio kula tu bali kufunga vitu vyote vinavyokupa furaha ya muda kuna faida kubwa sana hasa kwa wale wenye ukomavu wa juu wa upeo/ufahamu/uelewa.
Ukiingia ndani sana/za ndani sana kufunga ni sawasawa na kuu-factory reset mwili ili uanze upya katika hali yake ya kawaida iliyotakiwa iwe, kuanzia mabadiliko ya tabia(mental perception) , utendaji kazi wa mwili-kikemikali na kibiolojia (physiological), ((DETOXIFICATION))
Kumbuka uhalisia wa mazingira sio halisi bali ule uhalisia unaouona ni unatengenezwa na miili yetu (yaani ubongo) mfano unapoona kitu kitamu au kichungu ni ubongo ndio una tafsiri ile radha, hii inamaana uki-deal na mwili wako vizuri, utabadirisha mitazamo na namna ya ku deal na mambo tofauti tofauti.
Kufunga ni sawasawa na ku jailbreak mfumo mbaya uliouzoea (uraibu na tabia nyingine za ajabu) na kurudi katika mfumo wako wa awali kipindi unazaliwa.
Kiufupi ukifunga unaenda ku-clear ile brain reward system (Dopamine Fasting) vitu vyote ulivyo kua umevizoea na vimeanza kukutawala uraibu (addiction) kwa kipindi cha kuanzia siku 21 hadi 40 kumbukumbu yake katika ubongo zinafutika.
Itategemea na aina ya uraibu na umekua sugu kwa kiwango gani kuna wengine inabidi wafunge siku 40 hadi 70, na kuifikia mfungo wa siku hizo bila kufanya starehe kubwa sometimes usiingie hata kwenye social media (kitu chochote kinachofanya Dopamine hormone itumike kupita kawaida),
Utaona mabadiliko na utakua na uwezo mkubwa wa kubadili mtindo wa maisha(lifestyle) kama tu ule wa mwazo ulikua unakugharimu.
Kipindi cha feasting mwili najira inafikia hatua kiwango cha sumu mwilini kinapungua (accumulated toxic substances kupitia vyakula na vinywaji/vivuto hali inayopelekea hata antenna ya mwili kiwa safi na kuweza kudaka mawimbi kutoka ulimwengu mwingine(kiroho).