WESTGATE MASSACRE: 41 YEARS KENYA's STILL BEHIND

WESTGATE MASSACRE: 41 YEARS KENYA's STILL BEHIND

mossad007

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
1,165
Reaction score
852
Nilidhani baada ya Miaka takribani 41 since makosa yaliyofanyika baada ya matokeo ya Ugaidi kule Munich 1972 kwenye Winter Olympic Games Kenya watakua wamejifunza namna ya kukabiliana na ugaidi lakini wenzetu bado sana.

Kuna vipengele vichache ambavyo Ujerumani ilivikosea na kusababisha Wanariadha 11 wa Kiisrael kupoteza maisha na leo nashuhudia Kenya wakirudia kitu kile kile.

1. Role of Media Coverage

Kutokana na kukua kwa Uhuru wa Habari kwa wenzetu ( Europe ) baada tu Kikundi cha Black September kuwateka wanamichezo wa kiisrael media zilifurika nje ya Apartment waliyotekwa na kuanza kuripoti mwenendo mzima wa tukio. Ndani ya zile apartment kulikua na tv ambazo wale magaidi walikua wanaona na kufuatilia kila kitu. Matokeo yake Rescue Mission ya kwanza iliyopangwa na Polisi (hawakua na counter terrorism unit kipindi hicho) ikawa inapigwa picha live na wale magaidi wanona ni nini kinaendelea.

Ilikuwa kichekesho sababu magaidi waliweza kujua polisi wako wapi na wanafanya nini kwa kupitia tv zao ndani. Mission was aborted baada ya polisi kuona asilimia za ushindi kua chache. Leo wakenya wanafanya kitu kile kile updates zote ziko on air na kwa mujibu wa mashuhuda westgate complex ina dozens of tv sets ni km pale Mliman city tu unapoingia Game!

2. Rescue Team

Kikosi kilichopelekwa kufanya Rescue kinatoka KDF: Maroon Commandos (counter terrorism Unit) ukisoma Article moja online ya hawa jamaa wamesifiwa sana kua ni total replica ya their counterparts the likes of Sayeret Matkal (israel), NAVY SEALS (USA) and SAS (UK) cz huko ndiko wanako watrain. Lakini honestly speaking hawa jamaa wako nyuma kuliko ilivyosemwa cz kwa mission km hizi choice of weapons ina matter sana.

Counter terrorism zote ndani ya majengo au vehicles including ndege hufanywa kwa priority ya Mini Assault Rifles refer operation Entebe, Spring of Youth, Air Sabena (Sayeret Matkal), Operation Barras, Iran Embassy Siege (SAS) na Operation Bin Laden, (SEALS). Mini assault rifles hapa nazungumzia the likes of Heckler and Kotch, Uzi, Mini Galil, AK-74 folding etc. Ambazo ni ndogo, fupi, hubebeka kirahisi na zina range ile ile ya Weapons za kawaida hutumika pia na Makomandoo wa JWTZ km ilivyoonekana juzi Goma na kipindi cha miaka 50 ya Uhuru pale Taifa.

Lakini nimeshangaa kuwaona KDF: Maroon Commandos wakiwa wamebeba mitutu mirefu, mizito ya M 16 na zile Ranger Rifles za kiingereza tena za kizamani kwenye mission inayowalazimu wepesi na tacktics... its so absurd. Moja kati ya vitu vilivyotolewa duku duku na kamati maalum iliyoundwa after failure in Munich Massacre ilikua ni choice of weapons baada ya Polisi wa kijerumani kutumia Rifles kubwa zinazo punguza Manurvability and accuracy na kuundwa kwa special counter terror unit.

Kwa waliopitia mafunzo watakubaliana na mimi kua Counter Terror Rescue Mission ni zaid ya Uwanja wa Vita cz huokoi maisha yako tu bali na ya mateka na mali. Hivyo SPEED, ACCURACY and TIME are key elements. Ukimkosa gaidi kwa risasi moja analipua jengo zima ni matter of seconds tu ila vitani unaweza ukamimina ile Minimi mpka mkanda ukaisha na bado usiue mtu ukawa hai na wala wewe usife mkatupiana njugu mwezi mzima lakini hii sio sawa kbsa kwenye Rescue Missions ndio maana Choice ya Weapon hata mtu wa kuifanya hiyo kazi inamata sana... nilidhani leo wakenya watakua wamejifunza.

Mwisho kwa yaliyotokea Kenya hata TZ yaweza tokea hivyo tuwe makini na Siasa zetu za Kimataifa na kuboresha Ulinzi katika nyanja zote.

POLE ZANGU KWA WAHANGA!
 
mossad007 I totally conquer with you. There were so many tactical faults which the Kenya's Security Forces used and eventually led to the austerity, inhumanity and huge massacre of hostage who could be saved. I totally believe the failed rescue mission could at least catch attackers who managed to operate and move out of the scene live and safely. Unfortunately, no identification, control nor monitoring exercise for hostages who moved out were done. So it was easy for some attackers to take advantage of moving out.
 
Well explained! KDF and the rescue team failed absolutely, no doubt about it. Let them sharpen their minds before next catastrophe.
 
hivi walishindwa nini kuzima umeme usiku na kuiacha Mall iwe giza ili waingie na silaha huku wakiwa wamevaa night vision goggles au heat vision goggles

huku waki
move, five meter spread, no sound. double pack, heads up
 
mara ya kwanza nilivyokuwa naona wanajeshi wa kenya walivyobeba zile AK na M16 nilidhani lengo lao lilikuwa ni kuwazuga watu waliokuwa wanatazama.
lakini kadri muda ulivyokuwa unaenda nikajua ndio uwezo wao ulipofikia.
Sio Kenya tuu, nina wasiwasi hata sisi hapa kwetu huenda mambo ni yale yale tuu.
 
Nimeipenda post yako, ina facts na millitary techniques zilizosappotiwa na mifano halisi lakini zaidi history of past rescue missions and their success, failure, strength and weaknesses! Its more than informative, literally we can label it educative.
 
Kwanza uliona kumbe kuna raia tu wa kawaida aliejitolea na kuweza okoa watu?

hii inathibitisha jinsi gani hata security ilivyokuwa loose
yaani mtu tu katoka nyumbani kaamua kwenda kumsaidia kaka yake mule
huku polisi na hilo jeshi wanajishauri cha kufanya
hili jeshi la Kenya way hopeless....kuliko nilivyozania..
 
good analysis hata ukiangalia KDF hawakuwa na gears za maana zaidi ya kutisha watu na kifaru..
uvaaji wao na equipment pia sababu huwezi kuwa kwenye suicide mission na bunduki ina magazine moja tu..
 
Mimi nilipoona Uhuru anaongea kwenye TV body language na facial expression nikajua something went seriously wrong!!!!!

Ni makosa makubwa sana , kama waliona hawana uwezo kwanini hawakuomba msaada kutoka kwa wengine???
 
mossad007 I totally conquer with you. There were so many tactical faults which the Kenya's Security Forces used and eventually led to the austerity, inhumanity and huge massacre of hostage who could be saved. I totally believe the failed rescue mission could at least catch attackers who managed to operate and move out of the scene live and safely. Unfortunately, no identification, control nor monitoring exercise for hostages who moved out were done. So it was easy for some attackers to take advantage of moving out.

Everything was in shambles and the Kenyan security forces looked lost!!!

I am very dissapointed with the way Kenya handled that matter!
 
Naumia pamoja na waloumia wengine ila ukweli lazima usemwe. Kenya, i mean NIS in particular failed to strategize on this na ndo maana walikuwa caught off guard. Imagine naambiwa inawezekana magaidi walitorokea kwenye mfereji wa maji machafu (according to NTV's speculations) wakati KDF wakiwa busy kwenye media. Nilidhani walipaswa kusoma masterplan nzima ya Westgate ili kuziba namna yoyote ya kutorokea but hili halikufanyika zaidi ya kuwa hewani na helcopters ambazo hazikusaidia. Na kuziba barabara as if gaidi angekuwa mjinga kiasi cha kuwalk out majestically.

On this Kenya ilipigwa ngumi za usoni. But kubwa zaidi ni kwa jirani (TZ in particular) kujifunza na kuzuia kitu kama hiki kisitokee. Tupeane pole lakini ukweli tuuseme!

True Jamii Intelligence!
 
Halafu unaambiwa rais ndio amiri jeshi mkuu!!!!!

Kwa hili la majirani zetu mapungufu ni mengi mno na kama hii ndio hali halisi basi hao washambuliaji wanaweza kufanya ya "Olympus has fallen"
 
Kwanza uliona kumbe kuna raia tu wa kawaida aliejitolea na kuweza okoa watu?

hii inathibitisha jinsi gani hata security ilivyokuwa loose
yaani mtu tu katoka nyumbani kaamua kwenda kumsaidia kaka yake mule
huku polisi na hilo jeshi wanajishauri cha kufanya
hili jeshi la Kenya way hopeless....kuliko nilivyozania..

It was this dude sir mimi nilifikiri ni Polisi kumbe raia tu kajitolea na bastola yake na kaokoa watu wengi tu kuliko hata hao KDF wenyewe

good analysis hata ukiangalia KDF hawakuwa na gears za maana zaidi ya kutisha watu na kifaru..
uvaaji wao na equipment pia sababu huwezi kuwa kwenye suicide mission na bunduki ina magazine moja tu..

Nilikiri ni mimi tu nilikuwa najiuliza vile vifaru na magari ya Deraya ni vya nini? Yale magari ya Kivita yalienda kufanya nini pale wakati hata bastola tu zilikuwa zinatosha kuokoa watu kwa well trained and skilled task force lakini swali la msingi ni je sisi tunao ujuzi huo? Au likitokea la kutokea hata Kenya watakuwa na Afadhali sipati picha jinsi Kova atakavyoshinda mbele ya Kamera akitafuta sifa
 
Kwanza uliona kumbe kuna raia tu wa kawaida aliejitolea na kuweza okoa watu?

hii inathibitisha jinsi gani hata security ilivyokuwa loose
yaani mtu tu katoka nyumbani kaamua kwenda kumsaidia kaka yake mule
huku polisi na hilo jeshi wanajishauri cha kufanya
hili jeshi la Kenya way hopeless....kuliko nilivyozania..

Mkuu The Boss, sasa jeshi letu utaliweka kwenye category gani?
 
Back
Top Bottom