Weusi hawana mpango wa kusaini wasanii, sababu?

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,043
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka sababu za wao kutosaini wasanii.

Weusi

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kihasara’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kuamua kumsaini msanii ni kukubali kubeba ndoto zake zote alizonazo kitu ambacho kwa sasa hawapo tayari.

“Ukisema unafungua label au una kumsaiini mtu, ina maana anakukabidhi ndoto zake mikononi mwako, je unaweza kuzifikisha??, watu wanataka watengeneza maisha yao, sisi tunavyoona bado,” amesema Nikki wa Pili.

“Unamuona Chin Bees tumekuwa naye kitambo kwanini hatukumsaini lakini tumemsaidia mpaka amekuja kupata Wanene. Nikisema sasa hivi namsaini Chin Bees atanidai video kama tatu, atanidai promotion, hiyo itakuwa baadaye one step at a time,” ameongeza.

Nikki wa Pili ameshafanya kolabo tatu na Chin Bees ya kwanza ikiwa ni Role Model, Sweet Mangi na sasa Kihasara.
 
Inajulikana tu hao weusi ni matapeli wao wenyewe wanafanya ngoma bure wakidaiwa mpunga wanakimbia ndo waweze kumlipia msanii mchanga !
 
label kitu gani bhana hata shishi baby anayo. yani kila mtu ana label siku hizi kama fashion vile bila kujua maana halisi ya hii kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…