Kuna mkaka wa humu,alianza kama utani huko Pm,kama kawaida yao kwa kuomba namba ya WhatsApp walivyo fasta,akaniomba nikampa
Tumezidi kuwasiliana,na kuanza kuzoeana ingawa yeye yupo Dar ,na Mimi nikiwa Mwanza
Alianza kama marafiki,tukawa tunapiga stories za maisha hapa na pale,bila kuniambia kuwa ananihitaji kimapenzi
Sasa juzi kanitumia nauli nije huku Dar tukutane na kufahamiana zaidi,basi nikamwambia hamna shida
Nikaanza safari,kufika Dodoma ndo akaanza kuingiza stories za kulala pamoja,nikamwambia for first time haitawezekana,nitakuja huko tutaonana,basi siku nyingine nikija ndo tutafanya hivyo,akakubali
Nikafika hapa Dar,akanipokea fresh,akanipeleka hotel tukapata chakula,,ila akawa ananiomba tulale pamoja nikakataa,akalazimisha nikahisi nisipoweka kigingi kizito hapa naweza kuingia online bila matarajio
Basi nikamwambia,kesho yaani nipo tayari kwa hilo unalotaka ila sharti la kwanza tukapime magonjwa ya ngono,akakataa,nikamwambia basi nikachukulie chumba nikalale akaniuliza ila tutalala pamoja,nikamwambia wewe kachukue tutaongea huko chumbani,wakati ananyenyuka nikaita Tax nikasepa na kuzima sim
Haraka zenu muda mwingine mtakuwa mnaambulia zero,na kwa nini hutaki kupima zinaa kwanza,wengine tuna allergy na kondom,I'm sorry jamani,nipo nakata tiketi kwa ajili ya safari ya kesho
Mchango
========