Wewe mwanamke kuwa na huruma kwa mumeo

Wewe mwanamke kuwa na huruma kwa mumeo

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
Wanaume tunapitia maisha magumu sana, hebu fikiria mtu ambaye anafanya kazi, mnaishi wote halafu mwanamke anakuja kuvuruga kila kitu.

Nina jamaa yangu na mkewe wanaishi wote. Huyo mkewe alikuwa anafanya kazi zamani mkoa wa Mwanza na sasa hivi inasemekana amepata kazi Dar es Salaam hivyo kuhama kutoka Mwanza mpaka kuja kuishi jijini hapa.

Sasa yule jamaa yangu alisafiri zaidi ya mwezi akarudi, sasa nilivyomuona nikapata mshangao, kulikoni mbona amekuwa hivi, yaani mtu mchafu, hata anachoongea hakieleweki. Basi tukaachana.

Kesho yake akaja na mabegi mawili ya nguo, akayaweka ofisini kwetu, akasema anaelekea Morogoro lakini huyo mtu hana hata mia ya nauli.

Ghafla nikamuona ofisini mtu ana vumbi mwili mzima, sasa kwa wale watu wanaokesha wanasema alifika tokea saa saba usiku, alikaa hapa mpaka mnamkuta asubuhi hii.

Kwa kweli jamaa amechafuka, nikaanza kumuhoji nini kina msibu mpaka kufikia hatua hii?

Jamaa anasema ni mwanamke wake, anamnyima chakula, kulala, yaani hawana mawasiliano yeyote. Akazidi kuniambia ninavyomuona tokea atoke safari kwake hakuendeki ila anazurura, kula ndio kama hivyo tunamnunulia chakula.

Huyu jamaa anasema mbaya zaidi hela za benki huyu mwanamke katoa, gari kazuia, yaani hata hajui pakuanzia.

Kwa kifupi jamaa amechanganyikiwa, hata anachokiongea hakieleweki, anachokifanya hakieleweki.

Nilichogundua
Huyu alimuamini sana mkewe kiasi kwamba vitu vingi alimuandikia mkewe, hivyo mwanamke ameamua kubadilika na kumfukuza jamaa, mwishowe jamaa anajikuta hana kitu.

Wakristo tafuteni mfumo wa talaka.

Hawa watu wanapitia maisha ya hatari sana kwa jicho la tatu, huyu jamaa alisema mambo mazito sana.

Wanaume
Tuwe makini sana katika mapenzi, lolote linaweza kutokea hivyo tuwe makini katika mapenzi yetu, la sivyo unaweza fanya jambo baya sana kwa mwanamke.

Wanawake wamekuwa chanzo kikubwa sana kwenye kuharibu ndoa.

3335058428604770329.jpg.png
 
Nianze na suala la talaka kwa ndoa za kikristo. Kwanza hakuna talaka kwa ndoa hizo kulingana na vyapo vyake madhabahuni, ila siku hizi ndoa ikikorofisha na haina jinsi ya kurekebishwa wanandoa huoneshwa mlango wa kutokea kwa namna yake ambayo ni kwenda mahakamani kuvunja ndoa, na hii hufanywa na mwanandoa anayetaka kutoka.

Hapa kanisa halihusiki kuvunja ndoa, ila ushauri hutolewa na haohao wakubwa wa kanisa nje ya kanisa kama busara na hekima kuepusha shari na madhara mengine yanaweza kutokea endapo ndoa hiyo imeharibika na haiponyeki.

Mambo ya kuvumiliana mpaka kifo kiwatenganishe hayapo tena ikiwa kuna viashiria vya kutokea hatari kwa wanandoa au kuna tatizo la kimaumbile mwanandoa mmoja hawezi kufanya tendo la ndoa. Kwa habari ya uzinzi biblia imeweka wazi mwanamke mzinzi aachwe, labda ndio sababu ya kupelekana mahakamani kudaiana kugawana mali.

Mahakama nayo inataka uhalali wa ndoa ndio ivunje ndoa hiyo kisheria na mali zigawanywe kama zilipatikana wanandoa wakiwa pamoja. Ndoani ukiwa mpole utanyanyasika
 
Hapa umeleta majungu tu, fanyeni kazi mjipatie kipato, unaishi kwa kumtegemea mwanamke kisha unakuja kulialia hapa, yaani uwe na kipato chako na vyote hivyo umetafuta kwa juhudi zako halafu ulete upuuzinkama hui, vijana acheni UMALIOO mtakuja kufa shenzi kabisa
 
Back
Top Bottom