Habari wanajamvi,
Ninawashauri ndugu zangu wakati huu wa harakati za siasa kama kuna wezi au majambazi wamevamia mtaani kwenu na umepata upenyo wa kutoa taarifa polisi, piga simu na usema hivi;
"Kuna watu wanafanya kikao cha kujiandaa na operesheni UKUTA". Halafu wape ramani ya eneo la tukio.
Nakuhakikishia ndani ya sekunde chache utawaona wamefika.
Ila ukisema kuna wezi au majambazi. Mmmmh...