Wezi waiba nguzo 147 za fensi katika uwanja wa ndege Moshi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
1740849178738.jpg

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameagiza wezi walioiba nguzo 147 katika uwanja wa ndege Moshi pamoja na fensi waya kurejesha mara moja na kudai kuwa serikali haitafumbia macho wizi huo.

Babu ametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi mkoa, ambapo alisema kuwa serikali inaufanyia ukarabati uwanja huo wa ndege.

Alisema kuwa, Bilioni 12.5 zimetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo ambapo Bilioni 4 ni kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa uwanja huo.

Babu alisema kuwa, kabla Mkandarasi ambaye ni kampuni ya Rocktronic Ltd kukabidhi kazi ya ukarabati wapo watu wasio na nia njema wameiba nguzo 147 pamoja na kukata fensi waya na kuondoka nao.

"Waliofanya tukio hili ni Watanzania ambao hawana uchungu na hela zinazotolewa na serikali na nataka nguzo hizo pamoja na fensi waya kurejeshwa mara moja kwani serikali haitafumbia macho swala hili tutapambana na aliyepewa dhamana ya kulinda katika uwanja huo" Alisema Babu.

Akithibitisha kutokea kwa wizi huo, Mkurugenzi wa kampuni ya Rocktronic Ltd, Prajesh Chauhan alisema kuwa wamesharipoti swala hilo kituo cha Polisi Moshi kati kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
 
Hao vibaka Wakikamatwa, inabidi wahasiwe haraka sana.. ☹️☹️☹️
 
Tokea samia kushika nafasi ya uraisi mpaka wezi wa kuku wamerudi mtaani
 
Wizi na ufisadi ni masuala ya kawaida katika nchi zetu hizi.

Ripoti za CAG za Ukaguzi wa Mahesabu ya Mapato na Matumizi ya Serikali kila Mwaka zinaonyesha kwamba Wezi wamejuwa wakiiba mabilioni ya Fedha za Kodi za Wananchi kila Mwaka. Je, umeshawahi kuona hatua zozote zile kali zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya Wezi hao??

Prof. PLO Lumumba wa Kenya aliwahi kusema kwamba " Africa is dying because we are electing thieves to be the leaders in our countries."
 
View attachment 3255549
MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameagiza wezi walioiba nguzo 147 katika uwanja wa ndege Moshi pamoja na fensi waya kurejesha mara moja na kudai kuwa serikali haitafumbia macho wizi huo.

Babu ametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi mkoa, ambapo alisema kuwa serikali inaufanyia ukarabati uwanja huo wa ndege.

Alisema kuwa, Bilioni 12.5 zimetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo ambapo Bilioni 4 ni kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa uwanja huo.

Babu alisema kuwa, kabla Mkandarasi ambaye ni kampuni ya Rocktronic Ltd kukabidhi kazi ya ukarabati wapo watu wasio na nia njema wameiba nguzo 147 pamoja na kukata fensi waya na kuondoka nao.

"Waliofanya tukio hili ni Watanzania ambao hawana uchungu na hela zinazotolewa na serikali na nataka nguzo hizo pamoja na fensi waya kurejeshwa mara moja kwani serikali haitafumbia macho swala hili tutapambana na aliyepewa dhamana ya kulinda katika uwanja huo" Alisema Babu.

Akithibitisha kutokea kwa wizi huo, Mkurugenzi wa kampuni ya Rocktronic Ltd, Prajesh Chauhan alisema kuwa wamesharipoti swala hilo kituo cha Polisi Moshi kati kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mkuu wa mkoa anafuatilia wizi wa nguzo? Nchi ina maajabu hii. Polisi wanafanya nini? Mimi nadhani lengo kubwa la la mkuu wa mkoa lilikuwa kwenye hii sentensi ''Alisema kuwa, Bilioni 12.5 zimetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan''. Tunarudi kule kule. Niseme nini ili rais anione?
 
Kama mafisadi yanaiba kwa urefu wa kamba sembuse kwa walipa Kodi wenyewe!
 
Mtu anatoka zanzibar anakuwa mkuu wa mkoa bara hii ni maajabu 😡
Huyo ni Mzanzibari?

Kama ni kweli, basi nawashauri Watu wa CHADEMA waliangazie suala hili kwenye Kampeni zao za Siasa wanazofanya hapa nchini Tanzania ili kuchagiza ajenda yao ya No Reform No Election.

Walizungumzie suala hili kwenye mikutano yao ya hadhara.
 
Wizi na ufisadi ni masuala ya kawaida katika nchi zetu hizi.

Ripoti za CAG za Ukaguzi wa Mahesabu ya Mapato na Matumizi ya Serikali kila Mwaka zinaonyesha kwamba Wezi wamejuwa wakiiba mabilioni ya Fedha za Kodi za Wananchi kila Mwaka. Je, umeshawahi kuona hatua zozote zile kali zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya Wezi hao??

Prof. PLO Lumumba wa Kenya aliwahi kusema kwamba " Africa is dying because we are electing thieves to be the leaders in our countries."
PLO asikuzubaishe ana kiingereza kireeefu kisicho na maana..... lullaby English.
 
Back
Top Bottom