Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kaskazini mwa Msumbiji, mapigano yanaendelea na kuongezeka hali ambayo imelazimisha maelfu ya watu kutoroka makazi yao.
Sasa hivi idadi kubwa ya raia hao wanakimbilia nchi jirani ya Tanzania kulingana na mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani eneo la Kusini mwa Afrika alipozungumza na BBC.
Makadirio kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa na wadau wengine ni kwamba idadi ya kundi hilo la wakimbizi ni karibu watu 1000.
Aidha kulingana na Shirika la Chakula Duniani, sasa hivi serikali ya Tanzania ndio inayosimamia mahitaji ya kundi la wakimbizi walioingia nchini humo kutoka Msumbiji hivi majuzi.
Pia kuna taarifa kwamba unyanyasaji wa haki za binadamu katika eneo la Cabo Delgado umekuwa ukiongezeka huku mapigano kati ya wanamgambo wa Kiislamu na vikosi vya serikali yakiendelea.
Mpaka kati ya Msumbiji na Tanzania ni mto Ruvuma, na eneo la pwani ya bahari.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Msumbiji imeshuhudiwa idadi kubwa ya watu wakilazimika kutoroka makazi yao hasa katika mkoa wa Cabo Delgado huku wengine wakielekea eneo la kusini la Nampula, amesema mkurugenzi wa WFP.
Kulingana na Lola Castro mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani eneo la Kusini mwa Afrika, wiki kadhaa zilizopita Shirika hilo lilipata taarifa kwamba kulikuwa na kundi la watu lililovuka mpaka kutoka mto Ruvuma na kuingia eneo la Mtwara nchini Tanzania.
Inasemekana kwamba baadhi ya watu walitumia boti huku wengine wakiogolea katika mto Ruvuma kuingia nchini Tanzania.
''Usafiri ulizoeleka katika mto Ruvuma ni mtumbwi pia wanavuka kwa kutumia boti hadi visiwani eneo la delta la Msumbiji na Tanzania,'' amesema Lola Castro.