Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, linasema watu Milioni 2.4 wapo katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa nchini Kenya kufikia mwezi Novemba.
Tahadhari hii imetolewa wakati huu maeneo ya Kaskazini na Mashariki mwa nchi hiyo yakiendelea kukabiliwa na ukame.
WFP inasema, hali inatarajiwa kuwa mbaya na ni mara tatu zaidi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka uliopoita, wakati watu 852,000 waliporitiwa kukabiliwa na baa la njaa.
Shirika hilo sasa linaomba msaada wa Dola Milioni 139 kusaidia kukabiliana na majanga kama haya, lakini mpaka sasa ni Dola Milioni 28 ndio zilizopatikana kutoka kwa wahisani. Taifa hilo la Afrika Mashariki katika miaka ya hivi karibuni, imekabiliwa na majanga kma uvamizi wa nzige mwaka 2019, lakini pia ukosefu wa mvua ya kutosha kati ya mwaka 2020 na 2021.
Mwezi Septemba, rais Uhuru Kenyatta, alitangaza ukame kama janga la kitaifa huku mamilioni ya watu wakiendelea kukabiliwa na baa la njaa na kueleza kuwa serikali yake imetenga Dola Milioni 18 kuwasaidia wanaoathirika.