HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,567
Tunatatizo kubwa la maadin ktk nchi yetu, mambo machafu na maovu yana hamasishwa kwa nguvu nyingi.
Tunahitaji mabadiliko makubwa ili kuinusuru jamii.
Ukitaka kuthibitisha nachosema, subiri uone kuna watu hapahapa jamvini watakuja kukupinga na kuwatetea wanafunzi.
Subiri tu, utaona.
Unafikiri mahusiano yao kwa umri wao yana tija? Nini kifanyike kuwanusuru na hali hii?
Mkuu kuna mambo mengi ya kufanyika ila kwa halaka halaka ni ethics ni jambo muhimu sana na kwa sasa limepuuzwa.
Now days(?) a lot of students (age less than 18) try as much as possible to engage themselves into relationship of having a boyfriend and girlfriend. Na kwa sababu hiyo wamejikuta wakifeli na wengine hata kujinyonga baada ya kutendwa na wapenzi wao. Do they know what they real need in that kind of relationship …?
Nini kifanyike kunusuru hali hii?
Naomba mawazo yenu.
Next time andika kiswahili tu au lugha yako mama... kidhungu a.k.a kingleza achana nacho kwenye public utapata wachangiaji wengi lakini hivi wengine unatutoa kwenye mada kwa sababu ya lugha kuwa na sarufi yenye matege na makengeza kwa wakati mmoja!
Sawa, nakubali kukosoa na kukosolewa na ushauri wako ni mzuri na nimeukubali, lakini mchango wako juu ya hii topic ni mzuri zaidi ...
Nawakilisha ....
Sijui unasemaje hapo kuhusiana na mada
Mada yako ni sawa na inatoa nafasi kwetu sote kama sehemu ya jamii....lakini nadhani hata wewe unaweza ukawa na jibu zuri kwani huenda ulipitia hicho kipindi cha kujihusisha na mahusiano ya kimwili katika umri huo wa chini ya miaka 18! Lakini nadhani zote hizi zinatokana na jamii kuishi kwa kuiga kwani hao vijana wadogo wameiga vitu walivyokuwa wakiwaona wakubwa wao walipokuwa katika umri kama huo na wao wakawa wanatamani kushiriki, sasa umri kama huo unapotimia ndo hayo unayoyasema!
Kushusu kama mahusiano yao yanakuwa na tija au kama kweli wanajua wanachokitaka katika mahusiano hayo ni swala pana la ujana na kupevuka kwao! Huenda kwa kijana anayekuwa kwenye mahusiano anakuwa na tija kwa definition yake mwenyewe...ila wewe ambaye sasa ubongo wako umepanuka utakuwa unajaribu kudadisi tija ya mahusiano katika umri huo kwa mapana yake! Jibu zuri hasa unaweza kulipata kutoka kwa washauri wa rika!
Athari za mahusiano kwenye masomo pia ni swala lingine kwani kuna wengine wameshiriki sana kwenye mahusiano na bado wakafanya vizuri zaidi!
Umesema chini ya 18, hao wanataka kuexperiment zana zao, zaidi ya hapo ni hormone at its peak. Hakuna anayejua anachofanya au anachokitaka. Wewe unakunywa sumu kwa mtu mwenyewe kumbe analelewa na babake au kakuhadaa na kasimu kamchina.
Pili maadili ndio yametoweka, wazee inabidi wakaeni na watoto wao waelimishe kuhusu ukweli wa maisha. Ikibidi hata kumfundisha jinsi ya kujikinga na mimba au maradhi. Maana tunaishi kwenye utandawazi na kutokumweleza ukweli ni sawa na kuishi kwenye denial!
Hili suala la hormones ni visingizio, kwani wa zamani hawakuwa na hormones? mbona hawakufanya vituko kama vyetu?
Tukubali tu kuwa kizazi cha sasa kimemong'onyoa (kimepiga teke) yale maadili ya zamani yaliyokuwa yanapinga vitendo kama hivi. Kifupi jamii imehalalisha mambo haya!
Hapo kwenye bold ndugu yangu umenena vizuri sana. Na vipi kuhusu hayo maadilia ya zamani, yanaweza kujengwa tena kwenye kizazi hiki cha sasa ukizingatia na suala la changamoto za utandawazi na haki sawa mpaka kwa mtoto na wazazi wake wa kumzaa??
Hili suala la hormones ni visingizio, kwani wa zamani hawakuwa na hormones? mbona hawakufanya vituko kama vyetu?
Tukubali tu kuwa kizazi cha sasa kimemong'onyoa (kimepiga teke) yale maadili ya zamani yaliyokuwa yanapinga vitendo kama hivi. Kifupi jamii imehalalisha mambo haya!
Zamani walikuwa wanakeketwa