ha h aha,
hiyo ya u-lecturer nilikuwa sijaisikia ila sitashangaa. Waberoya kwake kila kitu kilichoharibika hapo Tanzania kimesababishwa na wapinzani.
Jana ulimbana kisawasawa aliposhindwa akanigeukia mimi akaanza zake za kulia lia nikamwambia kila hoja yako itajibiwa kwa hoja kadri itakavyokuja ana kasumba ya kuwabeza watu waliojitolea kwa mali na hali kuisaidia Tanzania kama kina Lipumba Mbowe Slaa Zitto Seif na wengine ndiyo hatukatai wana weakness zao tukimwambia aje na alternative anasema bora CCM sawa tuambie basi kwa nini iendelee hana jibu
Luteni,
Mimi nina motto yangu hapa JF, watu wenye viroja huwa siwajibu kwa hoja. Mimi huwajibu kwa hoja wale tu wenye kutoa hoja. Watu wenye udaku kama nikitaka kuwajibu namimi nawapatia udaku.
Kwa mfano -- watu kama mkamaP, kanda2 na wenzake huwa hawategemei kupata majibu ya kistaarabu toka kwangu kwa vile wanachoongea huwa ni upupu (kwa standard zangu). Kubwajinga/Waberoya and Co (yaani mamluki wa ccm) hapa pia hukutana na majibu yanayolingana na unafiki wao.
Nimesoma walichoendelea kuandika kwa zamu baada ya mimi kuondoka - (akianza mkamaP anakuja waberoya kabla kubwajinga hajaja kumalizia kabisa) nikacheka kama sina akili nzuri vile.
Hivi Msimbazi pake iko chini ya Mbunge wa ilala siyo?
Mzee Mwanakijiji!Hivi Msimbazi pake iko chini ya Mbunge wa ilala siyo?
Na hii hapa chini maeneo ya Msasani
Hapa ni njia ya kituo cha Polisi cha Msimbazi kama kinavyoonekana kwa mpiga picha. Nimepata picha hii toka kwa Evarist Chahali FB;
Ninajiuliza:
a. Uchafu huu ulianza kujirundika lini hapo? Ni wazi haikutokea siku moja ghafla bin vuup!
b. Ulipoanza kujirundika wahusika walikuwa wanafikiria nini? ni maua yanaota pembeni au mbolea?
c. Je kuna uwezekano wa wataalamu wa biolojia na viumbe hai kufanya utafiti kuona kama kuna jamii mpya ya viumbe hai imeanza kuishi humo na hivyo kutangaza eneo hilo kuwa ni hifadhi ya viumbe hai na kuwa ni "protected area"!?
d.Watu wanaoishi jirani na eneo hilo wanasubiri mwekezaji kutoka nchi gani kuja kuwasaidia kuwaonesha kuwa huo ni uchafu? au wanaamini "somebody's trash is someone's treasure"?
e. Inawezekana sisi ni taifa la watu waliozoea uchafu kiasi kwamba uwepo wake hautushtui tena kwani tumetengeneza some sort of immunity towards uchafu? Yaani hatuoni tatizo kupita na suti zetu, kupaki magari yetu na hata watoto kucheza mbele ya uchafu?
d. Do you see any similarity ya wananchi wa Tanzania na viongozi wabovu?
labda kufanya usafi wa namna hiyo kutawafanya watu waonekane kama "wazungu"..?
Kwani hakuna "wazungu" wachafu?
sijui kama kuna watu unaweza ukawaambia kule nyumbani kuwa wapo wazungu wachafu, ombaomba, wezi, wabakaji, wauaji n.k.. baadhi ya watu wanachukulia "uzungu" sawa na "ubora".. ndiyo maana wapo ng'ombe wa kizungu, kuku wa kizungu.. wanawake wa kizungu!??
Kumbe ndio maana kuna sehemu zinaitwa "uzunguni" na zingine zinaitwa "uswahilini". Na kumbe ndio maana ule msemo wa flani ana mambo ya "kiswahili" au flani ni "mswahili"....
Tuna matatizo mengi sana aiseee
Haswaaaaaaaaa,yule wa kuitwa ZUNGU!!!Hivi Msimbazi pake iko chini ya Mbunge wa ilala siyo?