Man U ya Fergie ilijizolea umaarufu kwa comebacks, sio comebacks tu but late late ones.
Comeback ambayo hawaitasahau mashabiki wa Man U, ni ile dhidi ya wapinzani wao wa jadi Liverpool pale OT kwenye kombe la FA raundi ya 4 mwaka wa Treble, 1999.
Owen anafunga goli la mapema, Dwirk Yorke anasawazisha dak. Ya 90, na super sub/Baby face assasin, Ole Gunnar Solskjaer anapiga goli la pili dak ya 92.
LAKINI, comeback ya UCL final dhidi ya Bayern Munich pale NOU CAMP, haisahaulika kirahisi na ni the best comeback ever kwa maana ya interval ndogo ya dakika zilizotumika kuiua Baryen Munich; Solskjaer tena, anafunga goli dakika ya 92+. Siwezi kuisahau hii!