What is your purpose in this life?

Mla Bata

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
7,841
Reaction score
17,491
Wasalaam,


What is your purpose in this life?

Have you ever asked yourself why are you living? Ushawahi kukaa peke yako ukazungumza na nafsi yako kujua ni ipi sababu ya wewe kuishi?

Wale wa mlengo wa kidini watasema wapo kwa ajili ya kumtumikia bwana/Allah na neno lipate kutimia but is that all?

I mean, honest speaking siku ambayo utaondoka kwenye uso huu wa dunia utapenda watu waliokufahamu, familia yako n.k likitajwa jina lako wakukumbuke kwa lipi?

Bado najiuliza kuna watu especially (Adults) ambao they don't have a life's purpose (s)? I know maana halisi ya maisha na malengo ya kuishi yametofautiana kati ya mtu na mtu kutegemea where you come from, uwezo wako wa kufikiri na kupambanua mambo, vipawa vyako ulivyoumbwa navyo n.k, ukiacha kuzaliwa kuishi na kufa kila binadamu ana dhumuni kuu aliloletwa nalo duniani, unaweza ukawa unafanya shughuli fulani kwenye maisha yako inayokupa kipato na kuendesha maisha yako lakini nafsi yako ikawa haina amani kabisa na jambo hilo na mwisho wa siku ukajikuta umeangukia kwenye lile lengo kuu na dhumuni la wewe kuishi.

Nakumbuka on my mid 20's wakati vijana wenzangu wa mjini mabaro baro wakiwa wanapambana kupata a basic lifestyle ya vijana wengi wa mjini kama kupata a fine and handsomely paying jobs, good apartments, a raving beauty and stunning girlfriends na kuenjoy maisha kila weekends, kwangu ilikuwa tofauti sana, moja sikuwa naeleweka, pili hivyo vitu kwangu havikuwa vipaumbele, maombi ya kazi nilikuwa sitaki hata kuyasikia na niliwapiga mpaka mikwala jamaa zangu wasinitumie hata hizo job applications πŸ˜…, wazazi na watu wakaribu wakahisi labda nimerogwa
(nakumbuka nishasikia kwa masikio yangu zaidi ya mara moja wazee wakiongea) "au wamemfanyia mambo ya kiswahili kijana wetu "πŸ˜‚,

Sikuwa na hofu wala wasiwasi sababu i had a clear picture of the things i needed in my life, and i knew exactly what it takes kufika ninapopataka na kuishi maisha ya ndoto zangu na kutimiza kusudio langu katika maisha yangu so sikuwa na pressure sana , it reached a moment it was a damn clear "jamaa kapoteza"
Vijana wenzangu (my close circle) tayari wakawa na familia (wake& watoto) ,mahusiano serious (uchumba), a well defined jobs,

wakati huo kwa upande wangu mambo yalikuwa tofauti kabisa ni kama vile tuseme kulia geuka watu wote wageuke kulia alafu peke yako ujikute umegeuka kushoto, now you know what i mean?

Ofcourse kibinadamu it doesn't feel good kuwa against everything lakini it was fine for me since i knew exactly what i wanted kwenye maisha yangu ni tofauti na wenzangu deep down ilikuwa inaniumiza hasa kwa upande wa familia nakumbuka nishawahi kumsikia mtoto wa my sister akisema waziwazi "nisome nigundue nini, wakati waliosoma kama uncle fulani maisha yao yenyewe hayaeleweki" 😨 that was too cold mf., yaani mimi ndio yule uncle asiyeeleweka kabisa kwenye familia,

kwanza i decided to stay a miles away from my home town ikawa kuonana na ndugu na familia ni mara mbili au moja kwa mwaka so hapo ndio wakawa hawanielewi kabisa, nikazidi kuwavuruga but personally nilikuwa kwenye kipindi muhimu cha mpito kufikia my life purpose, i gave myself a time, i was very patient, i stayed low as much as i could, and at the end of the day i earned my respect & appreciation and everyone came to understand ni nini nilikuwa nataka kwenye maisha yangu.

Well lengo ni kukukumbusha kuwa maisha unayoishi hayana maana yoyote kama hautakuwa na a purpose kwenye maisha yako, ukiwa na lengo lako kuu la kuishi au jambo unalopigania basi utaishi maisha kulipambania mpaka ulifikie na uliishi na utapolifikia basi hapo the whole meaning of your life utakuwa umeifikia, unless otherwise utakuwa unaishi ili mradi unakula na kushiba na kusubiri kufa tu.

What is your purpose in this life??? MY LIFE PURPOSE IS TO TRAVEL THIS WORLD! βœˆοΈπŸŒπŸ—Ί

"Everything is possible for those who believe" lets meet at the top, cheers πŸ₯‚.

Mla bata

MΓΌnchen, Deutschland πŸ‡©πŸ‡ͺ.
 
First things first, what is purpose?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…