"What is your salary expectation?"ni moja ya swali ninalolichukia toka kwa mwajiri

"What is your salary expectation?"ni moja ya swali ninalolichukia toka kwa mwajiri

Nyamalapa

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
211
Reaction score
469
Moja kati ya swali ninalolichukia toka kwa mwajiri ni "What is your salary expectation ?"

Huwa najiuliza kwanini mwajiri aniulize hivi wakati tayari ana scale yake kashaiandaa kwa position husika

Ni ngumu sana kumshawishi mwajiri aliepanga kukulipa 1,000,000 basic salary kisha akulipe 1,500,000 mana unakua uko nje ya bajeti yake.

Hili swali huwaga naona kama limekaa kimtego flani hivi, utaje kiasi kidogo ujipunje mwenyewe au utaje kiasi kikubwa mwajiri akuone kama una tamaa.

Binafsi nilikua naonelea ni bora waajiri kwenye kampuni binafsi wangekua wanafanya kama serikali kwamba tangazo la ajira linapotoka wanaweka scale ya mshahara kwa kila position kulingana na level yako ya elimu.

Mfano kampuni inahitaji ICT Officer, Operation Manager, Accountant n.k sio mbaya wangekua wanaweka wazi kiasi cha mshahara kwa kila post ili muombaji awe anajua kabisa kwamba hii kazi naaplai lakini malipo yake ni kiasi flani na kwa kufanya hivi watakua wanawapata watu ambao tayari washakubaliana na kiasi cha mshahara kilichopangwa hata kabla ya kufanya usaili.

Mana kuna muombaji mwingine wa ajira anatuma maombi kisha anaitwa kwenye usaili na kupata kazi lakini akija kutajiwa kiasi cha mshahara atakacholipwa anakua hayupo tayari kusaini mkataba mana inakua kinyume na matarajio yake.

Mtu alitegemea kulipwa 1,500,000 kama basic salary kisha unakuja kumtajia 700,000 kama basic kiukweli hawezi kukuelewa

Am done
 
Ukiona tangazo la kazi, lazima kunakua na kiwango cha mshahara na vigezo vinavyohitajika.
Sio matangazo yote ya ajira wanaweka wazi kiwango cha mshahara, wengi wanaweka tu vigezo vinavyohitajika ila malipo yanabaki kuwa siri yao.
 
Ni kampuni nyingi za bongo zinapenda kuonesha mshahara kama kitu confidential sana. Ila kampuni za nje unaona mzigo wako wote utakao pokea.

Mimi darasa la saba B nilikua nataja figure kama hawawezi tunakua tumemalizana
 
ukishaona umekua selected sehm em anza kuichimba iyokampun au taasis utendaj wao mishahara yaopromotions zao itakusaidia kua na cmfdenc unapokutana na panel ya intervie unakua kama unawajua kuna mgod wafanyakaz ktengo kmoja mishahara tofaut kisa ulvyotaja ndio wanaona huyu thamn yake na tukimpa alchoktaja atafanya kaz kwa weled lkn ukivuka exptetion yao ndio wanakupa basic waliopanga
 
Hilo swali ni la ma HR kujua kama una njaa utaje hela ndogo halafu hizo nyingine wazipige ukijichanganya tu imekula kwako
 
Back
Top Bottom