Ni mada nzuri,
Tujue jambo hili, Mke mwema au mme mwema, Mtu hupewa na Mungu haijalishi ana Elimu ya dunia hii kwa kiwango gani au hana! Muhimu ni kumtambua kuwa huyu ndiye mke wangu/mme wangu/mwenza wa kuishi naye.Matendo yake yatashabiana sana na matendo yako na pale ulipo na udhaifu mwenza wako atapabeba na hii ndo main object ya Mungu;kwamba udhaifu wangu basi Mke/Mme wako atakubeba, kwa mfano ukiwa mtu wa hasira basi ujue Mungu atakupa mke Mpole ili mwisho wa siku adesolve hiyo hasira kwa upole wake na muwe kitu kimoja yaani level mwili mmoja katika kupambanua na kufikia mwafaka.
Hakuna kitu kizuri kama Ndoa itokanayo na Mungu, huwa haizeeki ni mpya kila siku,ina upendo, ina uvumilivu, ina utii unaovutia hata watu wa nje.
Na kitu kibaya katika yote ambacho kimezaa yamkini mleta mada atakubaliana nami ni kitu kinaitwa kwa kimombo '' Proudness'' yaani kujiinua na kujifanya mmoja wao au Mke/Mme anajua kuliko mwingine hiyo ndo sumu ya Ndoa! Cha msingi kama Mungu amekupa Mwenza basi ujue hata kama hajasoma kwa Elimu unayotaka kwa mwonekano wako wewe basi kuna jambo nawe huna ufahamu nalo wewe ndo maana Mungu kakupa huyo Mke/ Mme ili kusawazisha mapungufu yako.
Elimu au Kazi au utajiri au umasikini we taja chochote unachokijua haviwezi kubeba nafasi ya Mke/Mwema maana vyote hivyo vimeshafanyiwa utafiti na vimeshindwa kabisa na ndoa zikasambaratika na taraka lukuki.Kinacholeta ndoa imara ni wewe mwenyewe kujua kuwa yuko Mungu awezaye kunipa Mke/Mme mwenye haiba niisikiayo nafsini mwangu na nitampenda kama nimpendavyo Mungu, nitamtii kama nimtiivyo Mungu,nitamvumilia kama ninavyovumilia kumgonjea Messiah! na kwa jinsi hiyo utampata hata kama ni Prof au Dr. au Master nawe ni msukuma mkokoteni kutakuwa na UPENDO wa dhati kumjali mwenzake kwa nafasi yake na Watu watawatambua kwa Matendo yenu.
Ref.Bible,Mithali 19;14,Efeso 5;28,33.
JF ninawaombea, mnaugusa sana Moyo wangu kwa fikra pevu na michango yenu ya Kimaadili na nadhani tutafika na ipo siku tutafika tufurahie matunda ya Nchi yetu.Zaidi nyote nawasihi ambao hamjaokoka basi OKOKENI wakati ndo huu.
Jone, Ndikupasya Buno Malafyale anganie kangi ambokie.
Ndaga.