What Made You Stay?

King'asti ubarikiwe sana haya mambo sijui lini watu watayaacha
kuna kisa kimoja cha kweli kabisa (lakini msikitungie Script) kinamhusu dada mmoja ninayemfahu.

Huyo dada baba yake alikufa yeye akiwa na miaka 13 na mama yake akiwa na miaka 27. Kwao walizaliwa watoto watatu yeye akiwa ni wa kwanza kuzaliwa. Baba yao alikuwa na wake wanne na mama yao alikuwa ni mama wa nyumbani anayetegemea kila kitu kutoka kwa baba yao. Siku ya kufa baba yao wao walikuwa wamepangishiwa nyumba kwa sababu mama yao alikuwa ni mke wa mwisho kuolewa kwa baba yao.

Kisa cha mama yao kuolewa na huyo baba ni kuwa alikwenda kutibiwa maradhi ya tumbo. Baada ya baba yao kufariki binti akiwa na miaka 13 na miezi kadhaa alianza kufanya biashara za kwenda minadani ambako alikutana na Tingo wa gari la mnadani na akiwa na miaka 14 na ushee akajifungua mtoto wake wa kwanza na kuhamia kwa huyo tingo. Tangu hapo ndipo mateso yalipoanza.

Akiwa na mimba ya mtoto wake wa pili aliwahi kupigwa kama mbwa na kutumbukizwa kwenye mfereji wa maji machafu mchana wa jua kali,kisa chenyewe eti mumewe alikuwa anamlazimisha awataje wapenzi wake wa zamani wakati kwa maelezo ya huyo binti jamaa ndiye aliiyefungua mlango wa "nyumba"

kuna wakati akiwa mjamzito alikuwa anashindia maji kwani jamaa alikuwa anasafiri hata kwa wiki mbili wakati siku ya kuondoka anajua ameacha buku mbili za matumizi lakini mwanamke akiomba hata maharage kwa jirani jamaa akijua hicho kipondo chake kama mwizi eti mwanamke anamdhalilisha na kumwaibisha.

Keshawahi kupasuliwa kichwani kwa chupa, mwilini ana mialama kibao ya kupigwa na kuchanwachanwa ama kwa kisu au viwembe. Jamii nzima inayowazunguka walifikia kuamini kwamba hayo ni mambo ya mapenzi ya watu wawili, Hata mwanamke apige kelele mara ngapi hakuna anayeingilia. mwanaume akaamini maisha ndiyo haya.

Siku moja jamaa karudi zake kutoka kwenye safari zake na nguo zake za Grease mwanamke kakaa kizingitini mwanaume akaanza kutuhumu "wewe jana umelala wapi? mwanamke kashangaa tuu "mbona mimi jana sikutoka kabisa kwenda popote tumbo lilikuwa linaniuma" jamaa kamwambia mwanamke aingie ndani. mwanamke katimua mbio, jamaa kufukuzia kwa nyuma hakumuona kumbe wasamaria wema wanawake wenzake wa jirani wamemficha chumbani kwao.Kaka mmoja mpangaji kwenye nyumba aliyokimbilia kuulizia na kuhadithiwa tukio zima akachukua jukumu la kumpangishia chumba siku hiyo hiyo na kumpa godoro na 100,000 ya kuanzia maisha.

miezi minne baadaye jamaa akaenda kumfanyia fujo kwenye nyumba ambayo amepanga na binti akaenda polisi jamaa akakamatwa na kuwekwa ndani. tangu siku hiyo adabu na heshima No fujo No kufuatiliana. Hatimaye binti kaolewa na bwana mwingine (siyo yule mpangaji) na sasa wana mtoto wa miaka 3 na wale aliozaa na yule bwana Bouncer wa kwanza mwenye miaka 19 yuko kwa baba yake na wa pili mwenye miaka 14 ni binti yuko kwa mama yake. Bouncer tangu waachane na huyu binti keshaoa na kuacha mara sita, Believe Me!!
 
kigarama,somo kubwa sana umetupa aisee! tabia hazibadiliki! kama alikua anampiga mwanamke mwingine (ujumbe kwa saram hapa),usidhani kua ww ni bingwa zaidi! usidhani ww utamnyenyekea vya kutosha. ni same as cheating, sio kama ukiwa small house,ukiwa promoted to big house ndo utakua tofauti!
the finest,unajua nikichangia thread hii nilikua nime-disable images, hiyo picha yako inanitia hasira kwa kweli! hapo,unaweza kusema kweli huyo mwanamke amebaki hapo kwa ajili ya hao watoto? like,is she doing them kids any favors?
 
Naweza kusema huyo dada alikuwa ana sifa ya uvumilivu kwa kweli maana mateso yote hai alipoamua kukimbia si kitu kidogo, halafu hapa ndio naona wale wanaume wenye tabia hii ni vigumu sana kuacha anaendelea nayo akipata mtu mwingine
 
King'asti sijui hata nisemeje mtu unapigwa mbele ya watoto wako, kama hawa watoto hawajaathirika kisaikolojia sijui kwa kweli maana hata mimi imeniwia vigumu sana kuandika mtu ambaye namfahamu alikuwa binti mzuri mwenye afya njema leo hii unamuona ana makovu ya mikanda kwenye mwwili wake yakiwemo ya visu, hata ukikaa naye ukiongea anachukua muda sana kukujibu sababu she's not herself anymore anachobakia kusema ni kuwa Mungu naomba unionyeshe njia, the only thing ambacho aliniuliza and i almost shed tears ni kuwa "Are you going to do the same thing to your wife when you get married". King'asti sijui kwa kweli i just wish you people could understand ni kitu gani nakieleza hapa regarding my friend i mean she has been traumatized, ngoja niishie tu hapa maana kuna kitu kimenishika kooni kinanifanya nisikie hasira
 
Kwakweli simulizi zote zinatia huruma sana; ila Faraja kubwa niliyoipata ni kuwa almost wanaume wote waliochangia huu Uzi wanasikitishwa na unyanyasaji huu!

Big up to you Real Men wa humu; you all will be blessed with happy homes! Love you all from my heart!
 
Kaunga i pray that God will show this woman a way and as well to all other women who are going through the same situation, it does hurt so much
 
Mhh!!! Inasikitisha sana pole MwanajamiiOne
 

Kweli Mbu malezi ni jambo la msingi sana la kuliangalia pia, maana akifanyiwa wa kwako lazima tuangalie mtu utajisikiaje
 
Mamushka nafikiri watu wanahitaji kujitambua wao ni nani na hatua anayokuwa amefikia inabidi kuchukua maamuzi bila kujali nani atasema nini na kitu gani

The Finest, unachosema ni kweli, kunasaa mtu inabidi ajilipue tu na kufanya maamuzi magumu sana kwenye life. Ila maamuzi ambayo yataleta manufaa mbeleni.
 

Ulichoongea ni point tupu kakaangu, tusipoamka wenyewe hakuna atakae tusaidia.
 

Halafu nimekumiso cha kukaa kimya hivyo, mzima kweli?
 

Mkuu thanks for your analysis maana hapa wote tunajifunza maana kwa hali ya namna hii kwa kweli it's so disappointing
 
Inasikitisha sana mambo haya yapo katika familia nyingi wengi wamekuwa hawasemi
 
inauma sana wanawake wengi wanapitia magumu ambayo hayaelezeki bahati mbaya hubadilisha maisha yao kabisa na sio lazima iwe kipigo
Kwa kweli Chauro inasikitisha sana ni wachache sana wanaoweza kuelezea unyama wanaofanyiwa ndani ya ndoa wengi wao wamekuwa ni waoga sana wanaishi chini ya hicho kivuli huku wakiendelea kupigwa kila kukicha
 
Hahaha!!! Tuko umenifanya nicheke asubuhi hii
 
JAmani polen wote mliotoa visa vyenu kwa wale wenye ndoa za furaha basi endeleeni kumshukuru mungu wale wenye ndoa zenye mateso Fanya maamuzi sahihi haraka iwezekanavyo,watoto isiwe kigeziokwan ukikaa hapo kwa kateso hayo na ukafa si wataishi tu? sembuse uhai ungalipo...say u can!kwa wale wenzangu na mie kama bado hujapata mwenza basi maombi ni silaha muhimu pia STOP and THINK before you enter in marriage!asanteni jamani nawapenda wote
 

hiyo picha imeniumiza sana na kunikumbusha mbali.siwezi kommenti from women's angle ila nikiwa mtoto niliishi kwenye familia ya hivyo....it's HELL!saa tisa usiku,mvua kali inapiga,mimi,my beautiful mama na my two sisters tuko kwa kiambaza cha nyumba tumezuia vichwa tu visilowe ila mili yetu ikitandikwa na mvua mercilessly sababu tu ndani hakukaliki kwa kipigo na manyanyaso!

it came a day ambapo nilitayarisha kisu changu kikali vizuri na nikasema moyoni 'leo akirudi saa saba na kuanza kutupiga sisi na mama i will stangle him to death...'.that day hakurudi kabisa nyumbani!sijui kwanini mama alichelewa kuondoka kwa yule mzee.nasikia aibu kwamba yeye ni baba yangu!
 
.hii mbaya sana,hivi ni kwa nini mungu naye anawapa waume binti kama angela?aende tu kwao,aachana nae huyo hafai
 
Mkuu pole sana kwa matatizo yaliyokupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…