What went wrong with Harmonize

Hilo nami nimeliona na nilishaanzisha thread humu hasa alipoanza kuwa sign wale madogo wa alikiba, nikasema Ibra hajamfikisha anapostahili halafu ana saini wengine wakati pia na yeye hafanyi vizuri kama awali. Nilishambuliwa wakiniita hater wengine wakisema mimi team WCB, wakati mimi nilikuwa ni mmoja wa wale waliomtakia kheri alipohama WCB nikiona kijana anajitafutia mafainikio zaidi.

Tatizo la nchi hii ni vigumu kutoa ushauri wa kujenga maana wananchi wanaamini katika mambo haya.

Ukisifia mazuri ya serikali wewe ni CCM na ukiponda wewe ni CHADEMA

Ukirekebisha Mabaya ya WCB basi wewe ni team ALikiba au Harmonize, na Ukisifia WCB wewe ni team DOmo and verse versa ndiyo ukweli.

Hakuna mtu kuwa neutral, yani watu tunatazama mambo kwa mlengo wa uteam tu.
 
Talent anayo , shida ni kuwa yupo confused , watu wanaomzunguka wanamshaur some how sivyo , naona kabisa kuna viashiria anaamini kabisa WCB wanapambana kumshusha na yeye kazi yake moja Tu ni kuwaoutclass , Kwa mazingira haya hawez kutoa hitsong zenye ladha , maana kutoa wimbo uliotulia inatakiwa uwe mentally relaxed ....
 
Ushamba unamsumbua bado ana akili za kampeni za uchaguzi. Na ndio jambo alilokuwa analiwaza sana mwaka huu.

Management yake ina political objectives nyingi sana. That's Control/management LOSS
 
Sijawahi kuwa na imani na management ya Harmonize, si watu wa music, ni wajasiriamali, hakuna kitu cha maana sana management wanaweza kufanya Konde gang, ndo mana kila kitu kinaishia juu mana kunakua hakuna execution plan... Kitendo cha kuanza kumponda Dai waziwazi huko ndo kufa kimuziki kwa Harmonize.
 
hapa hamna kitu. kutwa kushindana na diamond. hawazi tena kutunga nyimbo nzuri zaidi ya mashindano. ameshapotea njia
 
Harmonize amefanikiwa kule WCB kuna chawa watatu walikuwa wanamnyonya damu ...sasa hivi mpunga wote wake miendorsement ya kufa mtu..wanga wanatabia ya kutabiri uwongo
 
We uliingia jukwaa hili kufuata nn kama sio kufatilia maisha yao acha unafiki we mzee
 
Na tena ameachana na sarah(muitaliano)ndio rahisi sana kupotea anakurupuka sana asipojiangalia atapotea
 
Meneja wake ni manka toka kibosho,pembeni jembejembe wote wauza sura...hpo lazima ufeli tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…