Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi
Mjadala wa wasomi wa vyuo vikuu kujiunga VETA, unaendelea.
Nimejitolea kuwa a self appointed balozi wa dhana hii kuwaelimisha watu what it is!. Moja ya vitu vikubwa na muhimu ambavyo sisi Watanzania tunavikosa, ni uelimishaji umma kuhusu jambo lolote, kwa vile mimi ni muelimishaji umma, hili nimejitolea kilielimisha umma.
Angalizo kwa mode:
Jf ni user genereted forum, ambapo sisi user tuko huru kuanzisha mada yoyote kuhusu jambo lolote kwa kutumia lugha yoyote!.
Kadri jf inavyozidi kukua, sasa imekuwa kama main stream media, ukichanganya lugha, moderators wana translates na sometimes kupoteza maana kusudiwa.
Hii mada ina English Title,
Tanzania sio masikini, Tanzania ni nchi tajiri sana yenye Rasilimali lukuki, ila watu wake ni masikini kwa kukosa maarifa,ni umasikini wa fikra "Umasikini m-mbaya kabisa ni umasikini wa fikra"-JK Nyerere.
Nimegundua kumbe Watanzania wengi tuu, umasikini wao ni umasikini wa fikra, wakielimishwa kubadili mind set, na kujengewa uwezo wa kimitaji na mbinu za biashara, Watanzania wana uwezo mkubwa wa kumiliki uchumi wetu na kuwa mamilionea, na mabilionea!, kitu pekee walichokosa ni mitaji na mbinu za kisasa za biashara. VETA ni moja ya suluhisho la tatizo la ukosefu wa ajira。
Kila binadamu anazaliwa mtupu, bila kuja na kitu chochote hapa duniani, na siku anaondoka, anaondoka mtupu kama alivyozaliwa, hata akizikwa na jeneza la thamani gani, na kushehenezwa na vito vya thamani, dhahabu, almasi na vito, vyote vitaishia tuu pale kaburini, na kasha tuu la mwili, lakini mwenyewe anakuwa ameisha ondoka na haondoki na kitu chochote!.
Hivyo wote kama tumezaliwa watupu, utajiri na umasikini ni vitu tunavyovikuta hapa duniani na tutaviacha.
Kuna aina 5 za matajiri na utajiri, na aina 5 za masikini na umasikini, na umasikini m-baya kabisa ni umasikini wa fikra.
Aina 5 za Utajiri na Umasikini
Idadi ya Watanzania tunakwenda kufikia milioni 60!. Kati ya hawa kundi kubwa zaidi ni la masikini wa kutupwa wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea.
Ili tuendelee tunahitaji vitu 4, Land, labor, capital na entrepreneurship. Tanzania tuna land ya kutosha, tuna watu wenye nguvu, tumekosa capital na entrepreneurship. Umasikini m-baya kabisa ni umasikini wa fikra, umasikini wa mawazo ya kimasikini kuwa sisi ni masikini. Utafiti wangu binafsi umebaini Watanzania wengi ni watu wenye uwezo mkubwa, na wanamiliki ardhi ambayo ni mali, lakini hawana mbinu na mitaji.
Watanzania Tuna Uwezo wa Kuwa Mamilioneo na Mabilionea, Tatizo ni Mitaji na Elimu ya Biashara yaani entrepreneurship ambazo sasa zinafundishwa VETA!
Kunapotokea tatizo mahali, ili kulitatua hilo tatizo, hatua ya kwanza ni kulitambua tatizo, kukijua chanzo cha tatizo, kujua ufumbuzi wa tatizo hilo, na mwisho kuchukua hatua za kulitatua au kulifumbua. Tanzania tunakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira,unemployment。
Tukubali, tukatae, mfumo wetu wa elimu una matatizo, tunafundishwa elimu ya nadharia kwa kutumia modali za wenzetu ambayo imewajenga wasomi wetu kuajiriwa na sio kujiajiri au kujitegemea.
Mfumo wetu wa elimu, hatufundishiwi kutatua changamoto zetu bali ni elimu ya nadharia kubwa, lakini vitendo vichache.
Mfano Tanzania tuna elimu ya Fasihi, (literature), hadi Chuo Kikuu, tuna maprofesa wa Ph.D za fasihi makumi kwa mamia kutoka vyuo vikuu vyetu, toka miaka ya 60. Mimi nimesoma fasihi sekondari hadi Chuo Kikuu, hakuna hata kitabu kimoja cha fasihi kilichoandikwa na maprofesa wetu ambacho kilitumika kufundishia, vitabu vyote ni vya waandishi kutoka nchi za wenzetu!. Vitabu vya karibu ni ni vya majirani zetu wa Kenya, Ngungi wa Thiong'o, “The River Between” na Okot T’Bitek “Song of Lawino”, lakini tumefundishwa literature za Chinua Achebe “Things Fall Apart” na kina Henrik Ibsen “An Enemy of The People”, wote hawa ni waandishi wa nje, hivi hao wasomi wa Literature wa vyuo vyetu vikuu, wako wapi?!. Jibu ni wasomi wa nadhariia tuu!.
Nikiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), nilikuwa natembelea maktabu kuu ya UDSM, (ukiwa ni mwandishi wa habari, mwenye damu ya habari za uchunguzi, ukifika mahali popote, lazima tuu utachunguza hata kwa kupepesa macho). Sasa ukifika Maktaba ya Chuo Kikuu, sehemu za tasnifu za Ph.D, utakuta thesis za Ph.D mamia, zenye tafiti na majawabu ya matatizo yetu kwenye ma kabrasha yakila vumbi tuu maktaba, tafiti ambazo hazifanyiwi kazi!, kwa vile lengo la tafiti hizo ni tasnifu tuu za kupatia Ph.D, watafiti hao wakiisha tunukiwa Ph.D zao, kazi yao ndio imeishia hapo!, kilichotafitiwa kinaishia kwenye ma kabrasha!.
Ukifanyika utafiti wa mamilionea na mabilione 100 Tanzania, utashangaa kukuta nusu waliishia darasa la saba, na unaweza kukuta hakuna milioneo au bilionea yoyote ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu chetu!. Hii ni kwasababu tunafundisha elimu ya nadharia na sio elimu ya kujitegemea.
Bilionea mdogo kabisa kwa sasa ni Diamond Planinum, yeye aliishia darasa la 4!. Bilionea wa ukweli number moja wa Tanzania mwenye impact kubwa kwa maisha ya wengi, naomba nisimtaje jina, ila hakusoma hata darasa moja zaidi ya elimu ya madrasa!.
Hii maana yake, Tanzania hatuwezi kupata maendeleo ya kweli, kwa kuwategemea wasomi wa elimu ya kizungu ya darasani, tutapata maendeleo ya kweli kwa kuwajengea uwezo, Watanzania wenye vipaji vya biashara kwa kuwapatia mitaji.
Mwalimu Nyerere kwa kilijua, hilo, ali introduce elimu ya kujitegemea, ili mwanafunzi akimaliza darasa la saba aweze kujitemea. Mwalimu Nyerere alipomaliza kipindi chake, aliondoka, na siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea, Azimio la Arusha lenye Siasa ni Kilimo, Uhuru ni Kazi na Elimu ya Kujitegemea, vyote viliondoka nae.
Sasa tuna wasomi wengi wa chuo kikuu wasio na kazi za kuajiriwa,na kutokana na hicho walichosoma,hawajaweza kujiajiri, hivyo
Waziri Mkuu,Mhe。 Majaliwa Kassim Majaliwa amewashauri wakasome VETA ndio suluhisho!。

- What You Need
- What You Want
- What You Love
- What You Can,
- What is Available
- What You Get!,
- If You Can't Get What You Want, don't sit idle!
- Just Take Whay You Get!, grab it!
- Kisha tumia what you have to get what you love!
- Usongeshe maisha by Living your life to the fullest!, life is so short, muda ni mali!.
Tanzania sio masikini, Tanzania ni nchi tajiri sana yenye Rasilimali lukuki, ila watu wake ni masikini kwa kukosa maarifa,ni umasikini wa fikra "Umasikini m-mbaya kabisa ni umasikini wa fikra"-JK Nyerere.
Nimegundua kumbe Watanzania wengi tuu, umasikini wao ni umasikini wa fikra, wakielimishwa kubadili mind set, na kujengewa uwezo wa kimitaji na mbinu za biashara, Watanzania wana uwezo mkubwa wa kumiliki uchumi wetu na kuwa mamilionea, na mabilionea!, kitu pekee walichokosa ni mitaji na mbinu za kisasa za biashara. VETA ni moja ya suluhisho la tatizo la ukosefu wa ajira。
Kila binadamu anazaliwa mtupu, bila kuja na kitu chochote hapa duniani, na siku anaondoka, anaondoka mtupu kama alivyozaliwa, hata akizikwa na jeneza la thamani gani, na kushehenezwa na vito vya thamani, dhahabu, almasi na vito, vyote vitaishia tuu pale kaburini, na kasha tuu la mwili, lakini mwenyewe anakuwa ameisha ondoka na haondoki na kitu chochote!.
Hivyo wote kama tumezaliwa watupu, utajiri na umasikini ni vitu tunavyovikuta hapa duniani na tutaviacha.
Kuna aina 5 za matajiri na utajiri, na aina 5 za masikini na umasikini, na umasikini m-baya kabisa ni umasikini wa fikra.
Aina 5 za Utajiri na Umasikini
- Utajiri wa Kurithi- The Best Inheritors, umezaliwa kwenye familia tajiri, hivyo tangu unazaliwa wewe ni tajiri tayari, hata usipojishughulisha na jambo lolote, wewe utaishi vizuri kitajiri mpaka siku unakufa, wanaita umezaliwa na "silver spoon". Na ukizaliwa kwenye familia masikini wa kutupwa, mtaji wa masikini ni nguvu zake, usipofanya juhudi zozote kuibadili hali hiyo, au usipokuwa sehemu ya makundi manne haya yanayofuatia, then for sure, unazaliwa masikini na utakufa masikini!.
- The Best Talents- Hawa ni wale wanaozaliwa na kipaji. Hata kama umezaliwa kwenye umasikini lakini una kipaji, ukikitumia vizuri kipaji chako, kinakuletea utajiri, hawa ndio kina Michael Jackson, hakusoma hata darasa moja, Diamond Platnum aliishia darasa la 4!. Kwenye kundi la the best talents kuna wasanii, wanamichezo, wanamuziki wachoraji, waibaji, actors, etc. Na sisi Waandishi wa habari na Watangazaji tuko kundi hili. Kila mtu anazaliwa na kipaji fulani, ila wengi hawajitambui, hivyo wanakuwa masikini kwa kutokujitambua na kutumia vipaji vyao.
- The Best Brains- Hili ni kundi la wale bright, brilliants, genius, wenye akili nzuri, wanafanya vizuri darasani, wana score high, hivyo ku attract top jobs, kulipwa vizuri top salaries na hivyo kuishi vizuri, ma scientist, ma profesa, wasomi ndio kundi hili. Ila pia kuna wenye best brain ya akili tuu za darasani na kuajiriwa kulipwa mshahara, lakini hawana akili za maisha, hivyo baada ya kustaafu, maisha yanawapiga sana!. Hawa best brains ndio wasomi wetu wa chuo kikuu,ambao wamehitimu,wamekosa ajira,sasa tunawashauri bora waende VETA wakajifunze ufundi wajiajiri。
- The Hard Workers- Hili ni kundi la wafanyakazi kwa bidii, watu wanaojituma, wanatumia efforts zao na muscle powers zao kutoka jasho na kula kwa jasho lao, hivyo wanafanikiwa. Ukifanya kazi kwa bidii kwa kujituma, na kuwajibika, utafanikiwa, lakini ukipiga uvivu, lazima tuu utakuwa ni masikini wa kujitakia.
- The Fixers, hili ni kundi la watu wanaoendesha maisha yao kwa mishe mishe, they are well connected, they are not the inheritors, hawana talent yoyote!, they are not the best brains, wengine ni vilaza, they are not hard workers, but they have the best life. Kundi hili ndilo lenye wanasiasa, machawa na matapeli pia. Kwenye kundi hili kuna the lucky ones wenye bahati, wanapata connections, na channels, wanapiga pesa ndefu na wanakuwa mamilionea na na mabilionea. Hawa the lucky ones, baadhi yao wana kitu kinachoitwa "The Midas Touch" everything they touch turns to gold wengine wanasemekana wanatumia 'kizizi'!. The unlucky ones ni wasio na bahati, kila wanachofanya kinakwama, kinaishia njiani au kikifika mwisho hakizai matunda, hawa wanasemwa kuwa na damu ya kunguni, hata ukiwapa ng'ombe, akizaa, anazaa dume!.